Mashaytwaan Na Majini Wanaojiita Sharifu
SWALI:
Assalaam Allaykum
kwa nini mashetani ya kijini yanapenda kujinasibisha na Uislam?
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani kwa ndugu yetu muulizaji kuhusu mas-ala ya mashetani na majini. Shetani ni kiumbe kilicho asi maamrisho ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala). Anaweza kuwa ni binadamu au jinni, na ndio Allaah Aliyetukuka akasema:
((مِن شَرِّ الْوَسْوَاسِ الْخَنَّاسِ))
((الَّذِي يُوَسْوِسُ فِي صُدُورِ النَّاسِ))
((مِنَ الْجِنَّةِ وَ النَّاسِ))
))Na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas))
((Anayetia wasiwasi katika vifua vya watu)).
((Kutokana na majini na wanaadamu)) [114: 4 – 6 ]
Na kuhusu mashetani wa kibinadamu:
((وَإِذَا لَقُواْ الَّذِينَ آمَنُواْ قَالُواْ آمَنَّا وَإِذَا خَلَوْاْ إِلَى شَيَاطِينِهِمْ قَالُواْ إِنَّا مَعَكْمْ إِنَّمَا نَحْنُ مُسْتَهْزِؤُونَ))
))Na wanapokutana na walioamini husema: Tumeamini. Na wanapo kuwa peke
Tukirudi katika swali lako ni kuwa majini
Sasa majini wakiwa katika sehemu za Waislamu mara nyingi watajinasibisha na Uislamu na pia kujipatia majina ya Kiislamu. Na ikiwa watajipatia majina hayo basi wanaweza kusema wao wanatoka Makkah au Madiynah. Lakini hizo ni zao kwa ndimi zao na mara nyingi wanakuwa ni waongo kabisa.
Asilimia kubwa wanasema uwongo na nisba ndogo
Mfano mzuri ni ule wa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu 'anhu) aliyepatiwa jukumu la kulinda
Hivyo, mara nyingi wanasema uwongo hao mashetani kwa hivo usiwe ni mwenye kuwaamini hata wakisema nini.
Na Allaah Anajua zaidi