Chatine Ya Embe Mbichi
Chatine Ya Embe Mbichi
Vipimo
Embe Mbichi - 4
Pilipili mbichi - 2
Pilipili mbuzi - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) - 3 chembe
Chumvi - kiasi
Sukari - 2 vjiko vya chai
Namna Ya Kutayarisha
- Menya embe mbichi, katakata vipande vipande.
- Tia vitu vyote katika mashine ya kusagia (blender) tia saga kwa maji kidogo tu kiasi cha kusagia.
- Mimina katika bakuli ikiwa tayari kuliwa na chakula chochote upendacho.
