'Aqiyqah: Nani Mwenye Jukumu la Aqiyqah?
SW
Naomba ufafanuzi juu ya nani anapaswa kumfanyia aqiyqah mtoto, kwani kuna wanaosema ni jukumu la baba (kuumeni kwa mtoto). Mama haifai kumfanyia mtoto hata
Wabbillahi Tawfyq.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu 'Aqiyqah. Hakika ni kuwa jukumu la 'Aqiyqah limepatiwa baba mzazi wa mtoto. Jukumu
Ikiwa baba amekufa au kwa sababu moja au nyengine hana uwezo basi, mkewe anaweza kusaidia na ujira atapata mbele ya Allaah Aliyetukuka. Kwa hivyo katika suala hili kuna wasaa na kutegemea na maelewano yenu na kusaidiana kwenu. Kusaidiana ni njia njema kwani hata Maswahabiyah waliokuwa matajiri wakiwasaidia waume zao katika mambo kadhaa.
Kwa faida zaidi katika mas-ala ya ‘Aqiyqah ingia katika viungo vifuatavyo:
Kufanya Aqiyqa Ni Lazima Au Sunnah?
Umri Anaotakiwa Mtoto Mchanga Kunyolewa Nywele
Na Allaah Anajua zaidi