Aadam Na Hawwaa Waliteremshwa Wapi?

 

Aadam Na Hawwaa Waliteremshwa Wapi?

 

Alhidaaya.com

 

SWALI:

 

Asalam Aleykum Warahamatu Llahi Wabarakatu.                

 

Suala Langu Nauliza Hivi Huyu Adamu Na Hawa Walikuwa Ni Kabila Gani. Na Waliteremshwa Wapi. Hilo Ndio Suala Langu Kwa Hivo Natumaini Mutanijibu Vyema.

 

 

JIBU:

 

AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho

 

Kutobainishwa kwake ni maslahi kwetu kwani Allaah Aliyetukuka Hakuona umuhimu wowote juu ya suala hilo.

 

 

Kujua alikuwa kabila gani au aliteremshwa wapi haitatuongezea sisi Imani yetu. Kwa minajili hiyo, Allaah Aliyetukuka Akatuarifu kuwa Alimuumba Aadam kutokana na mchanganyiko wa udongo na maji na Hawwaa akaumbwa kutoka kwake (yaani bila ya kuwa na mama). Kwa hivyo, hatakuwa na kabila ambalo linafahamika.

 

 

Ama sehemu aliyoteremshwa anayoijua ni Allaah Aliyetukuka tu. Panasemwa ya kwamba aliteremshwa Kashmir lakini hakuna dalili ya hilo. Kitu ambacho kinajulikana ni kuwa yeye ndiye aliyejenga kwa mara ya kwanza Msikiti Mtukufu wa Makkah. Hivyo, inawezekana kuwa aliteremshwa hapo.

 

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share