Safari: Msafiri Kula Hadharani Wakati Wa Swawm Inafaa?
Msafiri Kula Hadharani Wakati Wa Swawm Inafaa?
SWALI:
Assalam alaykum warahmatullah wabarakat,swali langu linahusu swaum
safarini,mbili: uislam umekataza kula mchana hadharani mwezi wa ramadhan hata kama sheria inamruhusu mlaji mwenyewe,je muislam akiwa safarini ndani ya ndege ikafikia muda wa chakula na sheria imemruhusu kula mchana wa ramadhani,je atafanyaje?hali ya kua ndani ya ndege abiria wamejaa.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho
Ikiwa mtu yuko safarini katika chombo kama ndege, meli pamoja na wasafiri wengine, unaweza kula kinapoletwa chakula.
Lisilopasa ni kula hadharani mbele ya Waislamu wengine ambao wao hawako safarini, mfano wanaosafiri kwa gari na wakateremka katika mji na wakaazi wake wamefunga, kisha mtu huyo akawa anakula mbele yao. Inabidi ujitenge kula ili usiwatamanishe au kuwaweka katika hali ya kukutilia mashaka kwanini hufungi na ukajenga hisia mbaya baina yako na Waislam wenzako waliokuwa katika Swawm.
Na Allaah Anajua zaidi