Kwenda Kuswali Msikiti Ulio Mbali Kwa Ajili Ya Kufuata Qiraa Kizuri Au Khutbah Bora

 

SWALI:

Asalaamu aleykum,

Ningependa kuuliza suala ambalo baada ya rafiki yangu kunieleza kuwa haifai kuruka msikiti.Suala lenyewe nikua kuna msikiti dakika tatu kutoka kwangu lakini mimi napenda kwenda msiki uliopo dakika ishirini kutoka nilipo.
sababu inayo nifanya kupenda kwenye msikiti uliopo dakika 20 nikua nikiingia kwanza nasikia kweli nimeingia msikitini kisha siku ya ijumaa khutba inakuingia kisawasawa, huu mwengine pia kidogo baridi. lakini rafiki yangu aknieleza kua haifai kuruka msikiti, hii kidogo ilinibabaisha.
naomba usaidizi kidogo hapa.

Ahsante

 


JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Hakuna makatazo yoyote kuhusu hilo. Inapendezeka kuswali Msikiti wa karibu na kuimarisha Jamaa’ah iliyopo hapo na hususan kama Jamaa’ah ya hapo ni ndogo. Kadhaalika haipendezi kuruka Misikiti kuaacha wa karibu na kuufuata wa mbali kwa sababu tu ya kufuata Qiraa cha Imaam au Khutbah n.k. Kunaruhusika kuruka Msikiti endapo Msikiti wa karibu Imaam wake ni mtu wa bid'ah na hakusimamishwi Sunnah ndani yake, hapo unaweza kuufuata Msikiti unaosimamisha Sunnah japo uko mbali.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share