Anataka Kuoa Lakini Hajui Taratibu Za Kutafuta Mchumba Kisheria?
SW
Assalaamu alaikum.
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Na shukrani zetu kwa swali lako kuhusu taratibu za uchumba na kuoa. Hakika Uislamu umeweka utaratibu mzuri wa mvulana au msichana kutafuta wa pili wake katika maisha ya kindoa bila ya kupitia mifumo ambayo ni ya kumtweza mwenziwe.
Msichana pia anaweza kutafuta mchumba katika mipaka ya Uislamu bila ya kuwa na tatizo lolote lile. Hata hivyo, mara nyingi ni mvulana ndiye mwenye kutafuta mchumba kulingana na mipaka iliyowekwa na Uislamu. Ama kuhusu njia za Kiislamu za kutafuta mchumba zipo kadhaa na hapa tutaangazia kama mbili ambazo zinatumika
1. Kumjua msichana kwa njia moja au nyingine. Inawezekana umemjua kwa kuwa mlisoma Madrasah moja, au shule au chuo kimoja na ukamuona kulingana na nadharia yako ni msichana anayejistahi na kuchunga mipaka ya Dini. Hata hivyo, kwa sababu hamjaingiliana
2. Njia hii ni ile ambayo pindi mvulana anapokuwa tayari kuoa, anakaa chini na kuzungumza na mamake, dada zake, shangazi au halati zake na kuwaelezea lengo lake la kutaka kuoa. Hapo inabidi uwape sifa za mke unayemtaka na baada ya hapo watakutafutia mwenye sifa hizo kwani wao ndio wanaingiliana
Baada ya kuridhika na yale uliyoambiwa na katika uchaguzi huo, utaratibu unaofuata ni kuswali Swalah ya Istikhaarah na kisha kinachofuatia ni kupeleka posa kwa wazazi wa msichana na kuonana ana kwa ana na unayemposa. Kuonana huko si faragha bali uonane naye mbele ya maharimu yake. Ikiwa umeridhika na Dini na maadili yake na ukaridhishwa na umbile
Huku kuonana na huyo unayetaka kumuoa ni kwa mujibu wa nasiha aliyopatiwa Mughiyrah bin Shu'bah (Radhiya Allaah 'anhu) na Mtume (Swalla Allaahu 'Alayhi wa aalihi wa sallam), kwani kufanya hivyo kunajenga mapenzi. Wapo wanawake wengine ambao katika macho
Na Allaah Anajua zaidi