Kupokea Child Benefit Inafaa Na Ikiwa Analipa Tax Ya Serikali?

 

SWALI:

ASSALAM ALEIKUM,SHUKRAN KWA WEBSITE YENU YENYE MANUFAA NA MAFUNDISHO MBALIMBALI,ALLAH AWABARIK NYOTE MUNAOHUSIKA(AMIN). Swali langu ni hili je kupokea `child benefit` ni RIBA? au ni HARAM? Je kama utatumia kulipa `Council tax au nyumba?Tafadhali naomba jibu. Ahsante na wabillah taufiq.

Assalam aleikum, nashkuru sana kwa mawaedha na maneno mazuri kutoka kwa website yenu, Allah awajaalie kheir amin. Swali langu ni huku UK TUNAPOKEA `CILDBENEFIT`pesa hatukuzifanyia kazi, je itakua ni RIBA? Na kama ni RIBA, je tukizitumia kwa kulipa nyumba au maji itafaa? Please naomba munijibu maana hii ni mara ya tatu kutuma swali hili.Thanx. Maasalam.

 


JIBU:

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Kwanza tunapenda kukukumbusha wewe pamoja na waulizaji maswali wengine jambo ambalo tumeshaliwekea tangazo kwamba Alhidaaya inapokea maswali mengi mno, na watendaji wake ni wachache mno. Nasi tunajibu kwa zamu kwani hivyo ndio kumpa kila mtu haki yake. Hivyo tunawaomba muwe na subira hadi ifike zamu ya kujibiwa maswali yenu. Kutuma swali moja mara mbili au tatu haitosaidia kitu, bali ni kutuongezea kazi na kuzifanya hizi kazi zizidi kuwa ngumu. Tunaomba ushirikano wako na wa ndugu zetu wengine katika jambo hili.  

Child benefit ni miongoni mwa misaada kwa mwenye kutaka, halazimishwi mtu kuiomba bali inashajiishwa kuombwa, iliyojiwekea baadhi za serikali kuwasaidia raia wake wenye watoto bila ya kujali kipato cha raia hao wala mchango wao katika ulipaji wa tax. Ni msaada wenye sharti kubwa moja kuwepo kwa mtoto, hivyo basi kinachotazamwa ni mtu kuwa na mtoto anaeishi naye iwe wa kumzaa au wa kulea walio chini ya miaka 16 na wakati mwengine mpaka miaka 19 ikiwa bado wanaendelea na masomo yao ya kawaida, hivyo kuchukua, kuomba na kupokea child benefit si RIBA wala si HARAM na una hiari yako katika kutumia fedha ulizopewa ila kama utatumia kwa katika lengo lillilokusudia ndio vyema kwani lengo ni kukusaidia katika wanayohitajia watoto sio kulipa Council tax au nyumba au maji na bills nyengine.

Kipato chochote kile chenye kueleweka kama kipato kilichotokana na RIBA au kipato kilichotokana na HARAAM si halali kwako kukitumia katika jambo lolote lile wachilia mbali kulipa Council tax au nyumba au maji; kwani unakuwa bado unakula na kutumia riba au haraamu na hayo yote hayafai.

Na Allaah Anajua zaidi

Share