Saladi Ya Viazi Na Mchanganyiko Wa Mboga Kwa Mayonnaise
Saladi Ya Viazi Na Mchanganyiko Wa Mboga Kwa Mayonnaise
Vipimo
Viazi (mbatata) - 5 vitano
Ngegere, karoti - ½ kijiko cha kikombe
Maharage mabichi na mahindi mabichi - ½ kijiko cha kikombe
Mayonnaise - 5 Vijiko vya supu
Pilipili manga - ½ kijiko cha chai
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Menya viazi katakata vipande kisha changanya na vitu vyote vichemshe na chumvi kiasi
- Viache vipowe kisha mimina ndani ya bakuli kubwa.
- Changanya mayonnaise na pilipili manga tayari kuliwa na mkate au nyama ya kuchoma.
- Unaweza kuhifadhi kwenye friji kwa matumizi ya siku ya pili.