Pizza Ya Samaki
Vipimo
Tuna steki wa kopo (oiled) 180 – 185 g
Tomato ya kopo(paste) 3 Vijiko vya supu
Kitunguu maji 1
Chumvi 1 kijiko cha chai
Unga wa ngano 4 vikombe
Mafuta ya zaituni Nusu kikombe
Hamira 1 kijiko cha chai
Cheese ya Pizza 100 g
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Katika bakuli kubwa tia unga, hamira,mafuta na chumvi.Kisha mimina maji kidogo kidogo hadi mchanganyiko uwe donge la kunata kiasi tu.
- Funika na uwache unga kwa muda wa nusu saa kisha ukande tena kiasi ukijipaka mafuta mikononi, ufinike kwa muda wa masaa manne hadi sita.
- Ukishaumuka kufura itakuwa tayari kwa kuandalia vitu vya kuweka juu.
- Mimina tuna kwenye sahani huku ukichambua kuzidisha vijipande pande.
- Katakata kitunguu slesi nyembamba kando, tomato (paste) ndani ya kijibakuli tia maji vijiko 2 vya supu kisha koroga ili iwe kidogo nyepesi.
- Pake siagi au mafuta kiasi katika treya utakayochomea.
- Chukuwa unga ulioumuka ukande ufanye donge moja na limwagie unga mkavu.
- Litandaze donge kwenye treya mpaka upate chapati kubwa kwa mikono bila kutumia kifimbo.
- Mwagia tomato (paste) kwenye pizza utandaze ,kisha tuna halafu tupia vitunguu na utamalizia na cheese.
- Choma kwenye oveni kwa moto wa 200°C kwa muda wa dakika 25. Kisha unaweza kukata (shape) upendayo na itakuwa tayari kuliwa.
Kidokezo:
Ukipenda pilipili za kuwasha unaweza kuongezea na pia unaweza kutumia brokoli badala ya tuna.Ni vizuri kuliwa ikiwa moto moto.