Fatwaair Za Jibini Kwa Kunyunyizia Ufuta Na Habbat Sawdaa
Fatwaair Za Jibini Kwa Kunyunyizia Ufuta Na Habbat Sawdaa
Vipimo
Unga - 3 vikombe
Hamira - 1 kijiko cha kulia
Baking powder - ½ kijiko cha chai
Maziwa ya unga - ½ kikombe
Maji dafudafu (warm) - 1 kikombe
Mafuta au siagi - 1/3 kikombe
Sukari - 2 vijiko vya kulia
Yai - 1
Chumvi - ½ kijiko cha chai
Jibini (cheese) ya kukatakata - kiasi
Ufuta na habbah sawdaa (haba soda)- kiasi
Yai la kupakazia
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Changanya unga, hamira, maziwa, sukari, baking powder, chumvi.
- Katika kibakuli, changanya maziwa na maji yadafudafu (warm).
- Mimina maziwa katika unga, tia mafuta, na vitu vingine uchanganye vizuri na kukanda kidogo tu.
- Acha uumuke kiasi uwe saizi mara mbili yake.
- Fanya vidonge kisha sukuma uweke vipande vya jibini (cheese)
- Funga vikate kwa design upendavyo.
- Panga katika treya uliyopakaza siagi.
- Piga yai jengine vizuri kwa uma (fork) upakaze kwa brush kisha nyunyizia ufuta na habbah sawdaa.
- Pika (bake) katika moto wa 200 degrees takriban mpaka viwe rangi ya hudhurungi.
- Epua vitamu kwa chai.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)