Pizza Ya Sosi Ya Zaytuni, Nyanya Za Kukausha Juani (Sun-Dried Tomatoes)
Pizza Ya Sosi Ya Zaytuni, Nyanya Za Kukausha Juani (Sun-Dried Tomatoes)
Vipimo Vya Unga:
Unga wa ngano - 3 Vikombe vya chai
Chumvi - 1 1/2 Kijiko cha chai
Sukari - 3/4 Kijiko cha chai
Maji - 1 3/4 Vikombe vya chai
Hamira - 1 Kijiko cha chai kilichojaa
Mafuta ya zaytuni - 4 Vijiko vya supu
Vipimi Vya Sosi
Kitunguu maji – 2 katakata
Nyanya/tungule 3 saga
Nyanya kopo
Nyanya kavu za juani (Sun-dried tomatoes) – kiasi robo kikombe
Zaytuni (olives) – 1 kikombe (zikate slesi)
Oregano – kijiko cha chai
Chumvi kiasi
Pilipili manga – 1 kijiko cha chai
Mafuta – 3 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Unga:
- Changanya unga, pamoja na chumvi, sukari, na hamira, mafuta ya zaytuni katika machine ya kukandia.
- Tia maji kidogokidogo huku unachanganya mpaka unga ukandike vizuri na ulainike.
- Ufunike na uache uumuke kwa masaa 2 au zaidi.
- Washa oveni moto wa 440F.
Namna Ya Kupika Sosi Na Pizza
- Katika sufuria tia mafuta, ukaange kitunguu na nyanya hadi viwe laini.
- Tia nyanya ulosaga au ukate ndogo ndogo, tia nyanya kopo, na tia oregano, pilipili manga. Tia sun-drid tomatoes ulokatakata slesi.
- Unga ukishauumuka, katakata vidonge ufunue kutandaza kidogo kisha pakaza sosi, na mwagia zaytuni.
- Paka mafuta katika treya uchome (Bake) pizza hadi ziive.
- Epua zikiwa tayari
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kuburudika)