Amepokea Bidhaa Si Zake, Kuzifungua Ni Pombe, Afanyeje?
SWALI:
Mmi ni mfanyabiashara ya vitabu vya kiislamu. Siku moja nilinunua bidhaa, ikabidi nitangulie mzigo ufuatie baadae. Nilipofika ofisi ya gari nikakuta boksi lenye sura
Nilisita kuurudisha mpaka mwenyewe akaufuata. Mzigo wangu uliletwa kabla huyo jamaa hajaja. Jee ilikuwa niurudishe, niutupe au nifanyeje?
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu upokeaji wa bidhaa ambazo si zako.
Ifahamike kuwa Muislamu ni mtu ambaye yuko makini
Mbali na hayo, Muislamu anakuwa ni muaminifu na uaminifu unakuja hapa ni kuwa ulichukua mzigo wa watu kimakosa na hivyo unatakiwa umjulishe mwenye mzigo huo aufuate kuuchukua haraka kwani wewe kukaa nao pia haifai kwani ni katika mambo yaliyokatazwa kuyahifadhi Muislamu.
Tanbihi: Inatakiwa kama Waislamu tusaidianeni katika uchaji Mungu na wema wala tusisaidiane katika uadui na madhambi. Kwa minajili hiyo inatakiwa tuwe waangalifu
Na Allaah Anajua zaidi