Kutofunga Biashara Ijumaa Katika Nchi Isiyoongozwa Kiislamu

 

SWALI:

Iwapo Mimi mwenyewe na Wafanyakazi wangu wote Wanaowajibika na Ijumaa tumeacha biashara na kuitikia mwito wa Allah, isipokuwa wapo wale wasiowajibika na Ijumaa kama vile Mkristo, nikiacha aendelee kuwahudumia wenye dharura mbalimbli na wasiowajibika na Ijumaa kutakuwa na makosa? Kwa kauli ya Allah Wadharuw l'bay'a

 

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Shukran kwa swali lako kuhusu na nguzo muhimu sana ya Dini yetu nayo ni Swalah na hasa Swalah ya Ijumaa. Na kuhusu jambo hilo Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:

 

 

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِي لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَى ذِكْرِ اللَّهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ ذَلِكُمْ خَيْرٌ لَّكُمْ إِن كُنتُمْ تَعْلَمُون

 

 

“Enyi mlioamini! Ikiadhiniwa Swalah siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Allaah, na wacheni biashara. Hayo ni bora kwenu, lau kama mnajua”  [62: 9]

 

Hapa Allaah Anawahutubia walioamini, nao ndio wanaolazimika kwenda kwa ajili ya Swalah ya Ijumaa na wao ndio wanatakiwa wawe ni wenye kuacha na kufunga biashara kwa ajili ya kuwahi Swalah. Ikiwa wanaobaki katika biashara si wale ambao wanawajibika kuswali, biashara itakuwa haina tatizo lolote lakini ni bora zaidi kuifunga ikiwa wewe mwenye shughuli hiyo ni Muislamu.

 

Ni jambo la kusikitisha sana kuona ndugu zetu wengi Waislam wenye biashara zao wanashindwa hata kufunga kwa ule muda wa Swalah tu japo kwa nusu saa au lisaa limoja, na wakaenda kuswali, Swalah inawapita kwa tamaa ya kupata vijipesa viwili vitatu vinavyoweza kuwasababishia moto wa Jahannam (Allaah Atuepushe nao). Na hali hiyo ingawa Ulaya imeenea sana lakini hata Afrika na penginepo ipo vilevile.   

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

 

Share