Mwanamke Kutoga Tumbo Inafaa? Kama Haifai Kwa Nini Kutoga Masikio Na Pua Sio Vibaya?
Mwanamke Kutoga Tumbo Inafaa? Kama Haifai Kwa Nini Kutoga Masikio Na Pua Sio Vibaya?
SWALI:
Asalamu Alaikum, I just would like to know if belly piercing is haraam, and if it is why is the nose and ear piercing is not jazaki Llah kheri.
JIBU:
AlhamduliLLaah - Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na salamu zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho
Uislamu ni Dini yenye nidhamu na maagizo kemkemu ambayo yana maslahi makubwa kwa wanaadamu.
Kudunga au kutoboa pua, masikio au tumbo haifai kabisa kwa mwanamume aliye Muislamu. Ama kwa mwanamke Uislamu umeruhusu baadhi ya mapambo kama kutoboa masikio kwa ajili ya kutia kipuli na mapambo mengineo. Ama kwa tumbo, agizo ni, "Amewalaani Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) mwenye kuchanja – kutia chale (tattoo) na mwenye kuchanjwa, mwenye kuchonga meno na mwenye kuchongwa". Ikiwa kuchanjwa kumekatazwa seuze kujitoboa mwili.
Hivyo, kujitoboa masikio ni miongoni mwa mapambo kwa wanawake yanayojulikana na yaliyokubaliwa na wanachuoni ilhali tumbo si pambo na kwa hiyo haifai.
Shaykh ‘Abdullaah Jibriyn anasema, kutoboa tumbo ni katika mateso ya binafsi, na si sehemu inayotumiwa kupambwa na hakuna manufaa yoyote kw akitendo hicho, na isitoshe inaingia kwenye fungu la kubadilisha maumbile ya Allaah.
Na Allaah Anajua zaidi