Ummu Ayman (رضي الله عنها): Mama Muangalizi Wa Nabiy (صلى الله عليه وآله وسلم)
Kutoka Kitabu Cha: Sayyidaatu Mubashiraatu bil-Jannah (Wanawake Waliobashiriwa Pepo)
Mfasiri: Binti Ahmadah
MIMI NAULIZA, NA NINATARAJI KUWEPO JAWABU KUTOKA KWAKO KWA SUALA NINALOULIZA: JE WAKO WANAWAKE AMBAO WAMEBASHIRIWA PEPO? NA IKIWA LIPO JAMBO HILO, NATARAJI VILE VILE UNISIMULIE HABARI ZAO.
Nikasema: Ndio ewe mwanangu, wapo idadi ya Maswahaba wa kike. Wanawake ambao Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliwabashiria pepo. Na nimeazimia kukuarifu kila mmoja miongoni mwao. Kwa kila usiku insha Allaah nitakuhadithia kutokana na umuhimu wa sifa zao ambao waliishi wanawake hao.
Kwa hakika nimekusanya miongoni mwao Ummu Ayman, kwa sababu aliishi na kipenzi chetu, bwana wetu na kipozo cha uoni wetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakati wa utoto wake. Aliishi baada ya masiku ya uyatima wake uliokuwa mchungu.
Hii ni baada ya kupitisha Allaah kadhiya Yake kwa kufa baba yake bwana 'AbduLlaah bin 'Abdil-Mutwalib kabla ya kuingia kwake duniani.
Kisha akaondoka bibi Aamiynah bint Wahab kwa kuelekea kwenye uso wa Mola wake. Alimuacha mdogo aliyetimia miaka sita (6) katika umri wake akilia mbele ya kaburi la mama yake. Kikiumiza moyo kilio hicho na kuporomoka kwa shida za maisha.
Akamkimbilia Ummu Ayman kwa kumuhifadhi kwa utukufu wa Muumbaji, akamuweka bwana wa viumbe (Mtume) juu ya kifua chake na akimshika mikono yake na kumfuta. Na akimfanyia tahafifu kwa machungu yake ya msiba ambao ulifarikisha (kutenganisha) baina yake na mama yake katika wakati ambao alimuhitaji mno.
AKASEMA: LAKINI NINI KITAKUWA MBELE YAKE KWA UMMU AYMAN EWE BABA?
Nikasema: Hakika huyo jina lake ni Barakah bint Tha'alabah. Alikuwa akimsaidia bibi Aamiynah mama yake Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika mambo ya nyumbani kwake. Na baada ya kumaliza kipindi cha kumlea (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika ukoo wa banii Sa'ad, alimrejesha bibi Haliymah ambae alikuwa akimlea kwa ridhaa ya mama yake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) bibi Aamiynah. Na alikuwa Ummu Ayman akimuhifadhi na kumlea na kumuangalia kutokana na shughuli zote zilizokuwepo pembezoni mwa mama yake.
Na mara moja alitaka bibi Aamiynah kuzuru watu wake katika mji wa Yathrib (Madiynah). Akachukua katika ziara yake hiyo mwanawe pekee Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Ummu Ayman. Na baina yao katika njia wakiwa wanarejea, yakamjia maradhi bibi Aamiynah mbele ya kiunga karibu na Makkah. Na wala hakuweza kendelea katika safari yake yakamjia mauti na akafa na kuzikwa katika sehemu hiyo.
Wala hakuwa mbele yake Ummu Ayman ila ni kukibeba kitoto kilichofadhaika na kumpeleka mtoto huyo mpaka babu yake bwana 'Abdul-Mutwalib. Akaanza kumsimulia kwa yale yaliyomtokezea bibi Aamiynah. 'Abdul-Mutwalib Akamtaka Ummu Ayman amlee pamoja nae katika nyumba yake kama alivyokuwa akifanya katika uhai wa mama yake.
Alikuwa Ummu Ayman akimtumikia kwa ubora wa utumishi tofauti kabisa baina ya alivyokuwepo mama yake na baada ya kuondoka kwake. Alizidisha zaidi juhudi yake na alimfunika juu yake kwa upole na huruma, alifanya hivi kutokana na hofu juu yake na machungu kwa kutengana na mama yake. Alimpa hisia ya kwamba yeye hakuondokewa wala hatokutana na misukosuko kwa kufariki mama yake.
Aliishi yatima kitoto hichi kidogo katika nyumba ya babu yake bwana 'Abdul-Mutwalib kwa uangalizi wa Ummu Ayman na kutukuzwa na kukirimiwa kwa kuangaliwa kwa uzuri wa kumlea na ukarimu wa ulezi. Na kinyume chake yalimfika mauti pia babu yake bwana 'Abdul-Mutwalib. Kabla ya kukata roho, bwana 'Abdul-Mutwalib akausia kwa mwanawe Abu Twaalib kumlea Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Akafa 'Abdul-Mutwalib, akahama kipenzi kitukufu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na mlezi wake Ummu Ayman kuelekea katika nyumba ya Abu Twaalib. Na wala hakukuta katika maskani hiyo mpya isipokuwa ukaribishaji mzuri.
Alikuwa mke wa ami yake Abu Twaalib bibi Faatwimah bint Asad mwanamke mwenye upole wa kumkirimu Mtume. Mpaka akasema: Hakunipatia Abu Twaalib lililo bora kwangu mimi (kuliko malezi haya).
Ummu Ayman akamshuhudia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akikuwa hatua baada ya hatua hadi kuingia utu uzima. Na kwa hakika hisia za Ummu Ayman zilifanana na hisia za mtoto kwa mwanawe. Na alikuwa akihudumia katika nyumba ya Abu Twaalib kwa nafsi yake yote. Katika siku za Utume, alikuwa (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akisema kumwambia yeye: ((Hawa ndio watu waliobakia wa nyumbani kwetu.))
ALISEMA: NA NI KITU GANI KILITOKEZEA KWA KITOTO KILICHOKUWA YATIMA BAADA YA HAYO EWE BABA?
Nikasema: Baada ya kukua (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kulelewa, akaanza ami yake Abu Twaalib kufuatana naye katika baadhi ya safari zake za biashara.
Akasikia bibi Khadiyjah bint Khuwaylid juu ya uaminifu na ukweli wake Sayyidina Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Basi alisimama nae bibi huyo katika haki, na kukubali ujumbe wake wa kwenda Shaam kwa ajili ya biashara zake. Akimfuatisha pamoja na mfanyakazi wake Maysarah ili waweze kurafikiana.
Wakati aliporudi kwenye msafara, Maysarah alimsimulia bibi Khadiyjah aliyoyakuta kutokana na wema aliofungana nao bwana wetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na uaminifu wake. Na vipi walikuwa Malaika wakimfunika na kumlinda yeye na joto la jua. Akakubali bibi Khadiyjah kumwita Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kumtaka aje kumposa.
Baada ya kutimia ndoa hiyo ya vipenzi viwili hivyo, yaani bibi Khadiyjah na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), alipata utulivu Ummu Ayman ya kwamba Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amepambazukiwa katika uchungaji wa bibi mtukufu. Hajaufikia ubora wake cheo chake mwanamke yeyote miongoni mwa wanawake wa Ki-Quraysh, kutokana na kukubali kuolewa vile vile na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Ummu Ayman akachukua hadhi yake (ya kike) katika uhai wa kidunia. Akatanguliza mtumishi Ghabiyd bin Zayd mmoja miongoni mwa wanaotoka katika ukoo wa banii Haarith bin Khazraj kumposa Ummu Ayman. Akawafikiana Ummu Ayman juu ya ndoa hiyo, baada ya kutaka ruhusa kwa kipenzi kitukufu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ambae alitia baraka kutokana na hatua hiyo na furaha kubwa.
Ilikuwa hamu ya Ummu Ayman juu ya kusarifu kwa uchungaji wa mtukufu (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kushughulikia mambo yake, wakati alipopata utulivu juu yake na kuhakikisha anapata utulivu wa pahala kwa ndoa yake (bwana Mtume) kwa bibi wa Ki-Quraysh wa mwanzo. Akakuta juu ya kitu cha mwanzo katika uhai wake ameweza kukihakikisha. Na kutokana na hayo hatua yake ya pili juu ya kupata utulivu na kuanzisha ukoo wake.
Aliolewa Ummu Ayman na Ghabiyd na ikatowa matunda ndoa hiyo kwa kupata mtoto aliyeitwa Ayman. Na ilikuwa furaha kwa wazee wake wakubwa.
Akashusha wahyi Allaah Mtukufu Aliyetukuka kwa mjumbe Wake bwana wetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ujumbe wa Uislamu. Baada ya kulingania kwa siri, wakati Alipotuamrisha Allaah juu ya kuitangaza na kuita watu katika diyn mpya ya Kiislamu alipata uadui mkubwa na upinzani mkubwa hasa hasa kwa jamaa zake wa karibu. Akafa ‘ami yake na mkewe bibi Khadiyjah waliokuwa pembezoni mwake kwa kumsaidia na ilikuwa ni khayr kwa kumnusuru yeye. Na alikuwa bibi Khadiyjah wa mwanzo kuitikia wito wa Uislamu. Na alitilia nguvu Abu Twaalib juu ya kufungamana nae na kumlinda yeye kwa kila kitakachotokea kutokana na utukufu wake na cheo chake. Kwa sababu Ma-Quraysh walikuwa wakihifadhi kwa kutomuudhi Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ajili ya Abu Twaalib sehemu yake ya juu na uongozi wake na wakimkirimu kwa ukarimu wa juu.
Ummu Ayman na mumewe Ghabiyd bin Zayd walisilimu kwa pamoja. Wakachukua nafasi Ma-Quraysh kumfanyia maudhi kama ilivyo ada ya kumuudhi kila aliyemfuata bwana wetu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na kila aliyeacha diyn za baba zao na mababu zao.
Hapo nyuma, Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa akizuiliwa kuteswa kutokana na kinga aliyoipata kutoka kwa ami yake bwana Abu Twaalib. Baada ya kufariki ami yake, yalitokea yale ambayo asiyoyatarajia. Wakati huo huo alikosa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kipenzi cha kumnusuru au pakukimbilia kwake kutokana na kifo cha mkewe bibi Khadiyjah mama wa waumini. Abu Twaalib alianza kutangulia kwa kufariki kabla ya bibi Khadiyjah (Radhiya Allaahu ‘Anha). Hapo Ma-Quraysh walianza kuteremsha maudhi kwa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakapata wanayoyataka kutokana na fujo na kumzidishia mabalaa ya kila aina.
Wakati yalipozidi maudhi ya Ma-Quraysh juu ya Waislamu, aliwaruhusu Mjumbe wa Allaah kuhama kuelekea Yathrib (Madiynah) kila walipopata fursa ya kupenya usiku mara moja kutokana na shingo za Ma-Quraysh na wapumbavu wake. Na hayo ni kwa sababu Ma-Quraysh walikuwa wakiwazuia vijana kufuata diyn ya Uislamu. Wakiwaadhibu mpaka warudi nyuma katika diyn yao na kufuata miungu yao.
Na katika siku za ukame lilizidi joto, ikamuwia vigumu Ummu Ayman kuelekea Madiynah mji wenye nuru kwa ajili ya kuhama kwani alikuwa amefunga. Juu ya hivyo, alitoka Ummu Ayman bila ya chakula wala maji. Likaanza joto kumzidi, na kiu ikimzidi juu yake mpaka akafikia sehemu iliyoitwa Rauha – baina ya Makkah na Madiynah – zilipungua nguvu zake na ukaanguka ushupavu wake.
Akaanza kusinzia katika uwanja wa tabu. Akaanza kuona ndoo inaning’inia kwake yeye kutoka mbinguni iliyobeba kitu cheupe, mpaka ikafikia juu ya kifua chake. Akakimbilia kwa kuyapata maji yaliyokuwemo humo. Kisha akanywa na akanywa mpaka akamaliza kiu. Akahadithia Ummu Ayman kwa watu na akasema kwamba hakupata kiu tena baada ya kunywa maji hayo.
AKASEMA: ILIMFIKA KIU WAKATI WA FUNGA LAKINI NI VIPI ILIKUWA KIU YAKE?
Ndio ewe mwanangu, kwa hakika Alitambua Allaah fadhila zake kwake. Akahifadhi kwake yeye kudra yake, akasogezea maji kwa Ummu Ayman na Akaondosha kwake yeye kiu. Wala hayakuwa hayo isipokuwa ni takirima kutoka kwake Allaah kwa Ummu Ayman. Kwa kule kumfanyia ukarimu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wakati wa kumlea alipokuwa mdogo na kufuata ujumbe mkubwa aliokuja nao.
Wakati alipopata ruhusa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhama kuelekea Madiynah, alikuwa ni mwenye kuwakabili watu wake pamoja na waliohama ambao waliuacha mji wao wa Makkah kuelekea Madiynah. Mtume alisaidiana na wale waliohama pamoja na ndugu zao wa Ki-Answari kwa kujenga Msikiti ulio Mtukufu ambao aliuamrisha kuswaliwa baina yao. Mpaka pale lilipotimia jengo lake wakaanza Waislamu kuongoza kwa ajili ya kuwapita katika Swalah. Aliondosha tofauti zao Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Akanadi mwenye kunadi kwa ajili ya kutoka kwenda kupigana vita. Hakuna aliyekwenda kinyume na wito wake. Wakapata katika unyenyekevu- ama nusra ama shahada.
Wakati wa katika vita vya Khaybar, alitoka Ghabiyd bin Zayd pamoja na Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na maswahaba Waislamu kwa ajili ya kupigana na Mayahudi na kuwang’oa katika Khaybar kutokana na kuvunja kwao ahadi. Ama mkewe Ummu Ayman kwa hakika alitoka pamoja na idadi miongoni mwa Maswahaba wakiwa wasafi sio kwa kupigana, lakini kwa ajili ya kuwatibu majeruhi au kuwapa maji wapiganaji na kuwatayarishia chakula. Na ilikuwa furaha ya Ummu Ayman kwa kutelekeza wajibu huo, kwa hakika imefikia upeo. Na imekuwa ni wema wake usiokuwa na mpaka.
Akaingia ndani ya vita kwa ajili ya kuwanusuru Waislamu, na akandoka Ummu Ayman kwa ajili ya kumtafuta mumewe Ghabiyd kwa ajili ya kushirikiana katika furaha ya kuwashinda Mayahudi. Lakini wapi yalikuwa malengo yake?! Kwa hakika alikuwa Ghabiyd mmoja katika waliofuzu kwa shahada, na akapambazukiwa Ummu Ayman katika ujane.
Alipotambua hilo Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa yale yaliyomsibu yule aliyebeba ulezi wake yeye Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Alihuzunika kwa ajili yake na akamtembelea ili kumpa pole. Na alikuwa akirudia rudia ziara yake kwake Ummu Ayman. Hakuweza Ummu Ayman kuificha huzuni yake kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa mawazo ambayo yalimjaa katika nafsi yake.
Katika vikao vya (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) pamoja na Maswahaba zake watukufu, ilipita katika moyo wake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika kumfariji Ummu Ayman, akasema kuwaambia Maswahaba:
((Nani atamfurahishia kumuoa mwanamke anayetokana na watu wa peponi, basi amuoe Ummu Ayman)).
Bwana Zayd bin Haarith alikuwa ametengana na mkewe Zaynab bint Jahsh mtoto wa ‘ami yake Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Baada ya kupambazukiwa katika maisha yao wawili hao kwamba hawawezi kuishi pamoja.
Ama aliposikia Zayd maneno yale ya Mtume kuhusu Ummu Ayman. Hakuacha kukata tamaa hadi alipotia nia ya kupata utukufu wa ndoa kwa Ummu Ayman, na wala hakukubali kumfikia asiyekuwa yeye bwana Zayd.
Wala haikuwa kwa Ummu Ayman kwamba ni mzuri wa sura, bali ni kinyume chake. Alikuwa mweusi wa ngozi, na pua ya kulala. Lakini alikuwa na vitu viwili vya kuonewa wivu kwa kumlinganisha yeye: akiitwa Barakatan na pia akiitwa Ummu Ayman. Hakuna kitu chenye uzito na baraka kama binaadamu kuwemo katika ndoa.
Akaibariki Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ndoa hiyo ambayo imekusanya baina ya watu wawili ambao anawapenda na wa karibu nae. Akaishi Zayd pamoja na Ummu Ayman kwa uzuri katika masiku ya uhai wao. Na ikatoa matunda ndoa hiyo yenye baraka kwa matunda yenye khayr. Waliruzukiwa kwa du’aa ya Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa mtoto aliyeitwa kwa jina lake ni Usaamah. Akapambazukiwa Usaamah ni mwenye mapenzi juu ya mapenzi. Akaishi Usaamah pamoja na ndugu yake Ayman katika malezi ya wazazi wawili. Akalelewa na kushughulikiwa na mapenzi ya Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Ukabaki wema ukiendelea katika ukoo huo katika sura ya ukarimu. Mpaka ikafikia vita vya Mutta. Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akaliandaa jeshi lenye wasimamizi alfu thalathini (30,000) kwa ajili ya kupigana. Jeshi lililosheheni wapiganaji na viongozi madhubuti kabisa. Yamekuwa hayo kwa ajii ya kuwapiga Warumi - maadui wa Allaah.
Ilikuwa ni kawaida ya Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuweka juu ya kila kundi la majeshi kiongozi mmoja. Isipokuwa siku ya vita vya Mutta, kwa hakika alijaalia kwao wao viongozi watatu katika kila kundi la jeshi. Na akawapa habari ya kwamba kingozi mmoja wa mwanzo ni Zayd bin Haarith, ikiwa atapigwa basi kiongozi wa pili ni Ja'afar bin Abi Twaalib na akipigwa basi kiongozi wa tatu ni 'AbduLlaah bin Rawaah.
Wakakutana wapiganaji wote kwenye mkutano ambao zana hazikutosha za kupiganania. Wakakubaliana viongozi hao watatu juu ya kutegemeana katika mpangilio ambao aliupanga kwao wao Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kabla ya kutoka kwao kwa ajili ya vita. Na katika mji wa Madiynah uliteremka wahyi kwa Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika yaliyopita. Akasimama Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kutangaza kwa Waislam kwa mapenzi ya Zayd, bin Ja'afar na mtoto wa Rawaah. Bila ya kusahau kwamba Ummu Ayman amepambazukiwa na ujane kwa mara ya pili, hali ya kuwa waume zake wote wamefariki wakiwa ni mashaahid! Wala hakuwa Ummu Ayman mwenye kuomboleza isipokuwa ni mwenye matarajio na subra na kustaghafiru. Wala hakikuwa kifo cha mumewe wa pili ndio chanzo cha kukatisha uhai wake.
Alipotoka Mjumbe wa Allaah kwa ajili ya kupigana na washirikina katika vita vya Hunayn, alitoka pamoja nae Ayman, mwanae Ummu Ayman katika ndoa yake ya mwanzo pamoja na bwana Ghabiyd baada ya kukua kwake na kutimia ujana wake.
Kwa uwezo wa Allaah Aliyetukuka na Aliye juu, Ayman naye akashuhudia kwa kufa shahidi katika vita na kufuata njia ya baba yake na mume wa mama yake. Akasubiri bibi Barakah juu ya uamuzi wa Allaah, kwa hakika kulimsaidia yeye juu ya kuwa na iymaan kubwa na nguvu ambayo haikuteteruka juu ya jabali. Akasubiri hali ya kuwa amekwisha tanguliza vijana watatu aliowapandikiza mwenyewe ndani kutokana na kifua chake kwa ajili ya kupata radhi za Mola wake.
Lakini subra ya Ummu Ayman iliweza kuporomoka na azima yake na nguvu zote zilibomoka. Huo ni wakati ambao Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alitangaza kuwaaga wafuasi wake. Kwa hakika alihuzunika kwa huzuni isiyosemeka hadi kumkosesha fahamu za akili.
Kwa hakika amepokea Imaam Muslim katika Swahiyh yake Hadiyth iliyosimuliwa na Anas (Radhiya Allaahu ‘Anhu) amesema: Amesema Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘Anhu), baada ya kufa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliamrisha: ((Ni wajibu kwetu sisi kwa Ummu Ayman kumtembelea kama ilivyokuwa (kwangu).)) Alianza kulia na akasema kutwambia sisi: ((Nini kilichobakia? (Hakikubaki kitu) isipokuwa yaliyoko kwa Allaah (kifo) ni khayr kwa Mjumbe wake.))
Akasema Ummu Ayman: Kilichoniliza sio kwamba nilikuwa sijui juu ya kile Alichokikadiria Allaah ni khayr kwa Mjumbe wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Lakini ninalia kwa sababu wahyi umekwisha katika mbinguni. Isipokuwa ni kujishajiisha juu ya kile kilichobakia. Tukawa tunalia pamoja nae. [Swahiyh Muslim, 103/2454]
Kwa hakika Ummu Ayman alishuhudia uongozi wa Sayyidna 'Umar bin Al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ‘Anhu) na Khaliyfah huyo alimpa heshima yake namna alivyostahiki.
Na katika ukhalifa wa Sayyidna 'Uthmaan bin 'Affaan (Radhiya Allaahu ‘Anhu) Ummu Ayman alikwishaingia katika hali ya uzee na amepata utu uzima. Na imekwishamjia hali ya kuvunja ladha ya uhai pamoja na kutengana na jamaa zake.
Ikarejea nafsi yake kwa Mola wake iliyo radhi na yenye kuridhiwa. Kwa hakika ilikuwa kwake yeye ni mapumziko kutokana na safari ya umri uliokuwa mrefu pamoja na tabu na huzuni.
Amrehemu Allaah kwa barka Ummu Ayman na Ummu Usaamah kwa mapenzi na mapenzi ya hali ya juu. Akakutane nao mashahidi wake akiwa ni mwenye kung’ara na furaha. Amkutanishe Allaah pamoja na wacha Mungu wema miongoni mwa Maswahaba wa kike waliochaguliwa. AAMIYN!