'Aaishah (رضي الله عنها): Ndoa Changa Ya Mama Wa Waumini -3

Imetafsiriwa na Naaswir Haamid

 

 

Lawama Zinazotolewa Na Kufurahiwa

 

 

Binafsi na Waislamu wengi wengineo, ni lazima wasiwe na mshangao na namna ya viwango maradufu vinavyotolewa na Wakristo pale wanapolaumu mwenendo wa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kwa vile tumeshazisikia (lawama hizo) kwa muda mrefu mno.

 

Kuwa na mtu asiyesadiki Mungu, asadikiye kuwa hatuna habari za Mungu wala hatuwezi kuzipata – au mwengine yeyote asiyeamini kwenye msingi wa amri za maadili zinazotoka kwa Mungu – analaumu kitu ambacho “kisiasa si sahihi” kwa maadili ya viwango vya leo, ni vitu ambavyo havileti mshangao. Watu kama hao daima watapata kitu cha kulaumu, kwani wanaokota mfupa bila ya taabu kwenye “dini” kwa jumla.

 

Mazungumzo yote haya ya “maadili yaliyo kamilifu” yanapita njia yao kwa kujifurahisha, kwa hivyo wanataka kuifanyia dhihaka, kuitoa thamani na kuiondosha. Lawama za Wakristo, hata hivyo, ni jambo jengine. Wakati ni kweli kwamba Wakristo wanazungumza dhidi ya “uhusiano wa maadili” ambalo ni jambo linaloenea mno siku za leo miongoni mwa mataifa mengi yasiyo na dini, wao pia ni waathirika wasiojielewa wa jambo hilo.

 

Thamani ya Wakristo walio wengi hivi leo inatokana na heshima ya wanaharakati wa haki za binaadamu wa Ulaya ya Magharibi (au, kwa uchache, kwa kiwango kikubwa thamani yao inashinikizwa na wao). Thamani HAITOKI moja kwa moja nje ya Biblia – kifikra au kihalisia – bila ya kuangalia yale wanayoweza kudai. Kwamba Wakristo hivi leo wanajaribu kuibia kwa yale yanayoitwa “Uhuru”, “Haki za Binaadamu”, “Demokrasia” na “Haki za Wanawake” ndani ya Ulaya na Marekani si chochote ila ni dhihaka tu.

 

Inawezekana ikawaachia alama (ya mshangao) kwa wale wasiosoma ndani ya hizo nchi zinazoitwa – Nchi za Ulimwengu wa Tatu, lakini mtu yeyote aliyesoma historia anaelewa kwamba mambo haya yamekuja hata kwa kuwepo Kanisa, sio kwa sababu yake. Namna ambayo Wakristo wengi bila ya ujuzi wanachanganya heshima isiyo ya Kikristo (heshima inayodaiwa kuwepo) pamoja na thamani ya Bibilia daima imekuwa ikinivuta.

 

Mfano wa kwanza wa kushangaza ni namna utaifa na uzalendo vinavyotetewa miongoni mwa wengi wa madhehebu ya Wakristo Wanainjili Waliokoka (na) Wenye Msimamo Mkali (Evangelical Protestant) (na hata madhehebu mengine) ndani ya Marekani.

 

Uzalendo na Ukristo vinavyoenda sambamba ndani ya fikra za watu wengi, ni mfano tu wa namna tunavyoweza kumezwa kwenye “uhusiano wa kimaadili” bila ya kujielewa.

Kwa mujibu wa Uyahudi, Ukristo na Uislamu, zuri na baya ni amri za Mola Mtukufu. Kwa hilo, maadili hayabadiliki kwa wakati (huku) tukiegemea na matakwa yetu, hisia au uwepesi wa kujibu tamaduni. Ndani ya tamaduni ambazo hakuna hukumu za Kiungu katika jambo fulani, lipi zuri na lipi baya linaamuliwa kwa mujibu wa kanuni za utamaduni. Kwa mnasaba kama huo, mtu atatambua kuwa “sio maadili” iwapo ataenda kinyume na kanuni zilizokubaliwa na utamaduni wa jamii yake.

 

Kama tutakavyofafanua, ndoa ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha), ni tafsiri ya mambo mawili; yote kwa muongozo wa Utamaduni wa Mkamilifu na kanuni za utamaduni za wakati wake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kitendo hicho hakikuwa kinyume na maadili, lakini kilikuwa ni kitendo chenye mafunzo ya maana kwa vizazi vinavyofuata.

 

Kwa kuongezea, ndoa hii ilifuata kanuni za tamaduni za Mataifa yote ya Kishemi[1], zikiwemo zile za Kibiblia za wakati huo. Kwa msingi huu, na habari nyinginezo ambazo tutazitoa chini, ni unafiki wa hali ya juu kwa Wakristo kuilaumu ndoa ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) kwenye umri mdogo kama huo.

 

Kama wasomi wa Kikristo wapo ndani ya dhana za uongo kwamba thamani zao hivi leo zimepitwa na wakati na kwa upande fulani zinanasibiana na zile za wakati wa Biblia, tafadhali zingatia nukta zifuatazo ambazo moja kwa moja zinakwenda kwenye suala la; ni umri gani mtu anakuwa tayari kufunga ndoa:

·                   Kwa kuweka akilini fikra za “usahihifu wa kisiasa” na “maadili kamilifu”, ni wazi kwamba vipindi vya Biblia, umri ambao mtoto wa kike anaweza kuolewa ni kubaleghe. Hata hivyo, wakati wa Miaka ya Kati, kawaida ilikuwa ni miaka kumi na mbili. Sasa hivi, ndani ya nchi nyingi za “Kikristo” ni baina ya miaka kumi na nne na kumi na tano. Ninaishi ndani ya nchi ambayo baadhi ya mataifa yanaruhusu uhusiano wa jinsia moja kuoana kihalali, lakini wana nadharia ya kwamba kijana wa kiume wa umri wa miaka kumi na nane anayelala na binti wa miaka kumi na sita kuwa “mbakaji kwa mujibu wa sheria za nchi”. Kwa hivyo ingawa Wakristo wanaweza kutokubaliana na mengi ambayo yanajitokeza kuwa hayazuiliki ndani ya jamii za leo za Kimagharibi – ikiwa kwa utumiaji mbaya wa madawa ya kulevya, ndoa za mashoga au utoaji wa mimba – wao wenyewe wamemezwa (inawezekana bila ya kujitambua) na shetani lililo baya la “uhusiano wa kimaadili”. Bila ya shaka wao (Wakristo) watakuwa wanajisalimisha kwa kiwango kidogo kuliko watu ambao hawaamini msingi wa Uungu kwa maadili, lakini juu ya hivyo bado wanajisalimisha.
 

·                   Kwa mujibu wa historia, umri ambao umekuwa unatambulika kwa binti kuwa tayari kuolewa ni baleghe. Hii ndivyo ilivyokuwa kwa upande wa wakati wa Kibiblia, kama ambavyo tutajadili hapo chini, na bado unatumika kutambua umri wa ndoa duniani kote kwa jamii ambazo tamaduni za Magharibi zilizo fedhuli zinaziita “jamii za kale”. Namna ambavyo ahaadiyth kuhusu umri wa ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) inavyoonesha, ndoa yake ilifungwa angalau miaka mitatu kabla ya kuitimizwa kwa kitendo cha ndoa. Sababu ya hili ni kwamba walikuwa wakimsubiri afikie umri (yaani umri wa kuanza kutoka damu yake ya hedhi kwa mara ya mwanzo). Baleghe ni alama ya kiutabibu ambayo inayoonesha kwamba mwanamke anaweza kubeba watoto. Je! kuna mtu yeyote kwa kutumia akili anaweza kukataa hili? Sehemu ya hekima iliyopo ndani ya ndoa ya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) mara tu baada ya kufikia baleghe ni kuanzisha kisawasawa hili kama ni nukta ya Sheria ya Kiislamu, ingawa ilikuwa tayari ni kanuni ya kiutamaduni ndani ya jamii zote za Kishemi (ikiwemo ambayo Yesu (‘Alayhi swalaatu was-salaam) amekulia ndani yake). Wanazuoni walio wengi wa Kiislamu wanasema kwamba muda wa mwanzo ambao ndoa inaweza kutimizwa kwa tendo la ndoa ni mwanzo wa utimifu wa shahawa za ndoa (buluugh), kwa maana ya baleghe. Tokea ya kwamba hii ilikuwa ni kanuni ya jamii zote za Kishemi na bado ni kanuni kwa tamaduni nyingi za leo – hakika sio kitu ambacho Uislamu umevumbua. Hata hivyo, upinzani ulioenea hadi kwa kanuni zinazokubaliwa na za kihistoria za Kiuungu ni kitu ambacho bila ya shaka ni kipya!

 

·                   Lawama kuhusiana na ndoa ya Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) ni kitu ambacho ni kipya kwani kimekulia nje ya hadhi ya “Mara baada ya Uongofu” wa Ulaya. Hii ilikuwa ni Ulaya ambayo imeacha (au angalau kubadilisha) maadili yake ya dini kwa ajili ya seti mpya za heshima za wanaadamu ambazo wanaadamu wanatumia maoni yao wenyewe kutambuwa lipi zuri na baya. Unashangaa kuona kwamba Wakristo tokea hapo awali walilaumu (mara nyengine kwa dhana) tendo la Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) la ndoa ya mke zaidi ya mmoja, lakini sio ndoa yake kwa ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha). Bila ya shaka, wale wanaotoka asili ya Kishemi ya Mashariki ya Kati hawataona chochote cha kulaumu, kwa vile hakuna kitu kisicho cha kawaida au kisicho na maadili ambacho kimetokea. Walikuwa ni Wakristo wa Ulaya ambao walianza kumlaumu Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwenye nukta hii, sio wale ambao walikuwa wapo karibu na mizizi yao ya Kishemi.

 

·                   Ni pale ambapo mtu anafikia umri wa baleghe, mwanamme au mwanamke, ndio anakuwa na majukumu ya kisheria ndani ya Sheria ya Kiislamu. Kwa wakati huu, wanaruhusiwa kufanya maamuzi yao wenyewe na wanawajibishwa kwa matendo yao. Ni vyema iainishwe kwamba ndani ya Uislamu, si ruhusa kumlazimisha mtu kuingia kwenye ndoa na mtu ambaye hamtaki. Ushahidi unaonesha kwamba ndoa ya ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ilikuwa ambayo pande zote na koo zao zimekubaliana juu yake. Kwa msingi wa tamaduni zilizopo wakati huo, hakuna mtu ambaye ameona kosa lolote kutokana na ndoa hiyo. Na wakati huo huo, wote wawili walikuwa na furaha kuhusiana na ndoa hiyo.

 

·                   Hakuna vyanzo vya Waislamu vinavyosimulia kwamba mtu yeyote kutoka kwenye jamii ya wakati huo aliilaumu ndoa hii ambayo ilikuwa desturi kwa umri mchanga wa ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha). Kwa upande mwengine, ndoa ya ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha) kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ilihamasishwa kutoka kwa baba yake ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha); Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu), na ilikaribishwa kwa ujumla na jamii iliyo pana. Inasimuliwa kwamba wanawake waliotaka kumsaidia Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kama vile Khawlah bint al-Hakiim, alimuhamasisha kumuoa kijana ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘anha). Kutokana na tamaduni za Kishemi ambazo walikuwa wakiishi, hakika hawakuona kosa lolote kwa ndoa hiyo.

 

·                   Fikra za jamii kwenye mapenzi, koo na ndoa ni tofauti mno ndani ya hizo zinazoitwa (fikra za) Magharibi za leo ambazo ni za “kisasa” na “kistaarabu” kuliko wakati (fikra hizo) zilivyokuwa ndani ya wakati wa Biblia na Qur-aani. Bahati mbaya, wengi wetu tunabeba begi la “mapenzi ya mahaba” – “romantic love” na fikra kuhusu tendo la ndoa ambazo zimeweza kuzitia sumu akili zetu kwani Watu wa Ulaya (na fikra zao) zimeweza kuutawala ulimwengu. Fikra hizi sio tu kwamba zimepenya ndani ya fikra za Waislamu, lakini hakika wengi wao zimewalowesha (akili zao). Nguvu za kikoloni za Ulaya zimejiondosha takriban ndani ya ardhi zote za Waislamu, lakini ukoloni wa akili bado unaendelea! Kama tulivyoeleza hapo juu, sehemu ya huzuni zaidi ni kwamba watu wala hawatambui kwamba wapo chini ya hamasa isiyo ya Kiungu. Kidogo tu kutoa nukuu ya namna mambo yalivyobadilika, tamko ndani ya The New Encyclopaedia Britannica linaweka wazi kwamba hadhi kuhusiana na umri mwafaka wa ndoa umekuwa ukibadilika miaka baada ya miaka “...ndani ya Marekani na sehemu za Ulaya, kwenye mjumuiko wa hadhi ya watu wazima pamoja na waliopevuka kwenye tendo la ndoa kama ilivyoelezwa ndani ya msamiati wa kanuni ya dini katika kubaleghe haujakaribishwa.”[2]

 

·                   Ukweli wa kwamba tendo la ndoa na tabia za tendo la ndoa ya kuwa zinafanyiwa kazi ndani ya saikolojia ya mwanaadamu, una mizizi yake ndani ya mawazo ya Kifreudi. Hata mawazo yake mengi ya fikra za Freudi yanabishaniwa hivi leo, lakini bado fikra zake nyingi zina nafasi ndani ya mawazo ya watu wengi. Sigmund Freud (1856-1939) alifundisha kwamba wanaadamu kimsingi ni “viumbe vya tendo la ndoa” ambao msukumo wao wa shahawa kutokea utotoni ndio ufunguo wa kuelewa tabia zao. Ameanzisha utaratibu wa kuchunguza kwa kutumia saikolojia na fikra zake (yeye Freudi) kwenye tendo la ndoa, ukomeshaji wa kosa na tabia za tendo la ndoa, msukumo wa tendo la ndoa ambao hautambuliki vizuri akilini, fikra za Oedipus complex[3] na nyenginezo ambazo zimekaribia kuzoeleka ndani ya fikra za Magharibi kuhusiana na tendo la ndoa (takriban umbali wa dhana za ukosefu za Kanisa Katoliki la Kirumi). Wala hakuna haja ya kusema, fikra za Freudi zimekuwa zikilaumiwa kwa imani ya Wayahudi, Wakristo na Waislamu kwani kimsingi wanakataa jukumu la maadili ya mwanaadamu (kuchukua hatamu). Ndani ya fikra za Freudi katika vitu; viumbe hai ni wafungwa kwa athari ya kutotambua nguvu ya msukumo wa shahawa zao. Fikra hizo daima zinakaribishwa na “matakwa ya wananchi”, “wapiganaji wa haki za binaadamu” na mfano wa hao. Hata hivyo, kiini cha haya yote kwa mnasaba wa ndoa changa, bila ya shaka utatoa mwangaza hafifu. Kinachohitajiwa kuelezwa hapa ni mgongano wa “wanamamboleo” katika fikra za Kimagharibi kwenye tendo la ndoa. Wanarudishwa nyuma na mawazo ya ndoa kwenye umri wa kubaleghe, ingawa ni umri wa zama za kale. Hata hivyo, wana shule za juu high school ambazo elimu ya jinsia inafundishwa na jamii ambayo tabia ya tendo la ndoa imeenea mno dating na inatambuliwa kuwa ni maadili yao; mara nyingine, tendo la ndoa ni kawaida ya kufurahia hisia zinazokuja wenyewe za shahawa. Lakini mara nyingine ni tatizo la kisaikolojia kwani linapelekea athari mbaya zaidi. Kwa ufupi, kila kitu - kuanzia maisha binafsi hadi mifumo ya mahkama, zimeangukia kuwa ni waathirika wa mfanano wa maadili ya madaktari wa kisaikiatristi na kisaikolojia (madaktari kwenye nyanja za ubovu wa akili). Hali ambayo mtu anaweza kuishuhudia ndani ya maisha inawezekana kuwa ni namna ya “ukosefu wa akili” ambayo imeenea mno. Watu wengi wanaingia kwenye maisha ambayo wana imani thabiti kuhusiana na aina ya “mchanganyiko” ambao wameathirika nao kutokana na desturi ambazo wamezishuhudia ndani ya maisha yao ya kawaida yaliyo mnasaba. Utamaduni ambao unazalishwa na tabia kama hizo, kawaida, nyingi kati ya hizo zinapunguza makosa ya mwanaadamu. Watu ambao wametiwa hatiani juu ya jinai ambazo ni za hatari, badala ya kuwajibishwa kwa matendo yao, wao wenyewe wanatambulika kuwa ni “waathirika”, kwa vile tu wanafanya mambo ambayo akili zao zimejitengeneza hadi kuwasababishia kufanya hilo wanalolifanya.

 

 

 

 

 

 

[1] Taifa linalosemwa kutokana na Shem, hasa la Kiyahudi au Kiarabu [Mfasiri]

[2] Rites and Ceremonies” - “Kanuni za dini na Sherehe”, The New Encyclopaedia Britannica, toleo la 15 (1987), Juzuu ya 26, uk. 850.

 

[3] Ni jina na uchunguzi wa saikolojia ya Freudi na limepewa jina hilo baada ya hadithi za Kigiriki kwenye wasifu wa mtu anayeitwa Oedipus, ambaye bila ya kujitambua alimuua baba yake aitwaye Laius, na kumuoa mama yake mzazi Jocasta. Akijitokeza baina ya umri wa miaka mitatu au mitano, mtoto huyo anajiona kuwa na hisia za tendo la ndoa kwa mzazi wake wa jinsia tofauti na hamu ya kifo cha mzazi wake wa jinsia sawa. [Mfasiri]

 

Share