'Aaishah (رضي الله عنها): Ndoa Changa Ya Mama Wa Waumini -4
Imetafsiriwa na Naaswir Haamid
KUBALEGHE = KUPEVUKA = NDOA
Baadhi ya nukta hizo hapo juu zilizowasilishwa zina maelezo ya kina na ni vyema kuzifafanua. Kuna makala muhimu kuhusu umri ambao watu walikuwa wakioana kipindi cha Kibiblia ambayo ni Ancient Israelite Marriage Customs - Mila Za Ndoa Za Kale Za Wazayuni, kilichoandikwa na Jim West, ThD - Mkuu wa Ubatizaji. Makala hii inaeleza kwamba:
”Mke alitakiwa kutolewa nje ya ukoo (kawaida ni pale tu anapobaleghe au mnamo umri wa miaka 13) ili kuibakisha hadhi ya ukoo ukiwa safi.”
Huu ni ushahidi mmoja wapo wa ukweli kwamba inatambulika kwa vijana kuoana pale tu wanapobaleghe. Watu hao wa kipindi cha Kibiblia walikubaliana kuoana kipindi cha awali. Wakati tukijadili maana ya neno ‘almah, ambalo ni neno la Kihibruu kwa maana ya “mwanamwali” au “msichana aliye baleghe”,[5] Gerald Segal anasema:
“Hata hivyo, ni lazima itambulike kwamba, kipindi cha biblia wasichana waliolewa umri wa awali.”
Juu ya kuwa Magharibi wanazungumza kwa ufedhuli kana kwamba ni “tamaduni za kale”, lakini Kitabu cha An Overview of the World’s Religions - Muhtasari wa Dini Kuu Duniani kinaweka wazi kamba baleghe ni alama ya kale ya umri wa ukubwa:
“Takribani tamaduni zote za kale zinatilia mkazo kwenye ubaleghe na kanuni za ndoa, ingawa kuna tabia ya kutilia mkazo zaidi kwenye kanuni ya wavulana na wasichana. Kwa sababu ubaleghe na ndoa zinaashiria ukweli kwamba watoto wanashikilia majukumu ya utu uzima, tamaduni nyingi za kale zinatambua kuwa kanuni inayozunguka mazingira haya ni muhimu. Kawaida ya kanuni za kubaleghe zinakwenda sambamba na tafrija za kutahiriwa au (tafrija) nyengine za (kutahiri) uume. Ni nadra kutahiriwa kwa msichana, ingawa hilo linatokea kwa baadhi ya mila. Kanuni ya kubaleghe kwa msichana mara nyingi inahusishwa na pale anapoanza kutokwa mzunguko wa damu ya hedhi kwa binti mchanga.”
Baadhi ya waandishi wanawake wanakubaliana na hili:
“Baleghe inatafasiriwa kuwa ni umri au kipindi ambacho mtu kwa mara ya mwanzo anaweza kuzalisha mbegu za uzazi, kwa kuweka kumbukumbu ya hesabu hii, kuna kuwepo kanuni au sherehe kama ni sehemu ya tamaduni za kuweka kumbukumbu kwa tokeo hili kubwa.
“Kupata siku zako” inamaanisha kuwa ni njia na alama ya wanawake wachanga kuingia kwenye uuke. (Kutoka kwa Women’s Resource Center – Kituo cha Huduma cha Wanawake).”
Rejeo nyengine inayohusiana na ndoa katika umri wa baleghe ni makala kuhusiana na Afrika ya Kati, inayosema: “....wanawake wanaolewa mara tu baada ya kubaleghe”.[6] Nukuu zilizopita, na nyingine zaidi ya hizo ambazo hazikutajwa (ndani ya makala hii), ni lazima zithibitishe kwa mtu yeyote mwenye akili timamu kwa namna gani wataalamu wenye habari zote za binaadamu na wanahistoria wanavyotambua hadi leo: kwa karne zilizopita, watu wanatambulika kuwa wapo tayari kwa ajili ya ndoa pale wanapofikia baleghe.
Itambulike kwamba kutokana na maoni ya upande wa Kiislamu, matatizo mengi ya jamii ya leo yanaweza kuchunguzwa kuwa mzizi wake unatokana na kutupilia mbali ndoa za mapema. Kwa mujibu wa namna Mola Mtukufu Alivyomuumba mwanamume na mwanamke, yaani wakiwa na shahawa za hali ya juu, watu ni lazima waoane mapema. Huko nyuma, hili lilikuwa ni sahihi zaidi kwani matarajio ya umri wa kuishi ulikuwa upo chini (yaani unatambulika kuwa ni “mzee” kama utafikia umri wa miaka 40!). Sio tu kwamba ndoa inatoa mlango wa kutokea ulio halali kwa watu wenye afya nzuri, lakini ni kawaida kuwa inazalisha watoto zaidi. Lengo mojawapo la ndoa ni kuzalisha watoto. Hii ilikuwa ni muhimu zaidi huko kale, pale watu walipokuwa hawawezi kuishi kwa muda mrefu kama ambavyo wanavyoishi sasa na idadi ya vifo vya watoto wachanga vilikuwa vipo juu.
UMRI WA KUBALEGHE
Ingawa tumeeleza kwamba baleghe imekuwa ni alama ya kanuni ya kale, kiutamaduni na kidini kuonesha kuwa tayari kwa ndoa, baadhi ya watu wanaweza kuwaza ni katika umri gani baleghe inachukua nafasi. Hili kwa upande fulani halina mantiki kwa mnasaba wa mjadala wetu mahsusi wa Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘Anha), kwani simulizi ya Hadiyth inaonesha wazi kwamba alikuwa amefikia baleghe. Hata hivyo, kwa mjadala wa baleghe na umri gani wanawake wengi wanapata mzunguko wao wa damu ya hedhi, (tuangalie nini) anasema ‘Abdul-Haamid Swiddiqi:
Uislamu haukuweka kanuni ya kikwazo cha umri wa kuingia baleghe kwani inatofautiana baina ya nchi na tabaka kutokana na hali ya hewa, urithi, masharti ya kimwili na kijamii. Wale wanaoishi kwenye maeneo ya baridi wanachelewa zaidi kuingia katika baleghe ikilinganishwa na wale wanaoishi kwenye maeneo ya joto ambapo wavulana na wasichana wanapata baleghe kwenye umri wa awali.
“Wasitani wa hali ya hewa ya nchi au wilaya,” anasema mwandishi maarufu wa kitabu cha Woman - Mwanamke, “anatambulika kuwa ni kiini kikuu, kwa hapa sio tu kwa mnasaba wa hedhi lakini kwa mnasaba wa mwenendo wa shahawa wakati wa baleghe.”[7] Raciborski, Jaubert, Routh na wengine wengi wamekusanya na kuweka pamoja takwimu kwenye somo hilo zinazofafanuliwa kwa wasomaji. Marie Espino amefupisha baadhi ya takwimu hizi kama ifuatavyo: (a) Kiwango cha umri wa muonekano wa mwanzo kabisa wa hedhi ni baina ya umri wa miaka tisa na ishirini na nne kwenye maeneo ya baridi (b) Kiwango cha umri kinatofautiana mno na inawezekana ikakubalika kuwa namna ulivyo ukaribu wa mstari wa Ikweta, ndio ukaribu wa kiwango cha kufikia hedhi.[8]
Kwa kuongezea, makala yenye jina la Puberty in Girls – Ubaleghe kwa Wasichana ya Jumuiya ya Afya ya Jamii ya Serikali ya Australia, inasema: “Alama za awali za kubaleghe (ni) kukua ghafla: unaanza kuwa mrefu, chuchu zinajitokeza, nywele zinaanza kuota sehemu za siri na chini ya kwapa. Hii inaweza kuanzia baina ya miaka 10 hadi 14 – inawezekana ikawa mapema kwa baadhi na kuchelewa kwa wengine.” Makala ya Physical Changes in Girls During Puberty – Mabadiliko ya Mwili Kwa Wanawake Wakati Wa Kubaleghe ina haya ya kuzungumza;
“Wakati wa kubaleghe, mwili wa mwanamke unabadilika, ndani na nje, hadi ndani ya umbo la mwanamke. Mabadiliko hayo hayaji kwa mara moja, na hayajitokezi kwa wakati mmoja kwa watu wote. Wanawake wengi wanaanza kuonesha mabadiliko ya kimwili baina ya miaka 11, lakini kila mmoja ana ratiba yake ya kuendelea (kubadilika) kwa mujibu wa umbile lake la ndani. Ni kawaida ya mabadiliko kuanza mwanzo kabisa kama vile umri wa miaka 8 au 9, au yasitokezee kabisa hadi 13 au 14. Hata kama hakuna kinachoonekana au kuhisiwa kuwa kuna mabadiliko yoyote, mabadiliko yanaweza kuwa yameanza kutokea ndani ya mwili wako.”
Wengi wao watakubaliana kwa kusoma hapo juu kwenye maelezo hayo, lakini bado wapo ambao watashikilia na misimamo yao kuhusiana na iwapo ndoa ya mtu mzima inaweza kuwa ni changamfu kwa msichana mdogo. Tukiweka mbali dhana za Kimagharibi za “uchangamfu” kwa muda tu, ndoa ya ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘Anha) na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ilikuwa ni yenye furaha kwa wote na yenye mapenzi kama ilivyoelezwa ndani ya Hadiyth nyingi na vitabu vya Siyrah. Kwamba ndoa hiyo ya furaha ilikuwa ni ya uadilifu ingawa ni ya umri ulio tofauti, inatumbulika baina ya wanasaikolojia kuwa:
“Pale tofauti za (umri) ni kubwa, mfano kupindukia miaka kumi na tano hadi ishirini, matokeo yanaweza kuwa ni ya furaha zaidi. Ndoa ya mzee (msimamizi), bila ya shaka siyo ya mzee (dhaifu) kwa msichana mdogo, mara nyingi ni yenye mafaniko na ya hamasa. Ghafla Bi Harusi anazoea maingiliano ya kawaida na tendo la ndoa”[9]
HEKIMA ZAIDI ZILIZOPO NYUMA YA NDOA HII
Kwenye maoni yake ya ahaadiyth ndani ya Swahiyh Muslim ambayo imetaja kuhusu ndoa changa ya ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘Anha) kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), ‘Abdul-Haamid Siddiqi ameonesha nukta nyingine tatu za hoja ya kuwepo kwa ndoa hii:
- Ndoa ya ‘Aaishah kwa Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) katika kipindi cha umri wa mwanzo imemfanya Mama ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘Anha) kuwa ni shahidi wa karibu wa maelezo binafsi ya maisha ya Mtume na kuyabeba hadi vizazi vinavyofuata. Kutokana na kuwa karibu na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kiroho na kimaumbile, ndoa hiyo ilimtayarisha ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘Anha) kuwa ni mfano kwa Waislamu wote, haswa kwa wanawake, kwa vipindi vyote. Ameimarika kiroho, kiuwalimu na kiuwanazuoni, kwani alikuwa ni mwenye kipaji cha kupigiwa mfano cha akili na busara. Sifa zake zimetoa msaada kwa kazi ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na mbali zaidi ni sababu ya Uislamu. ‘Aaishah, Mama wa Waumini (Radhiya Allaahu ‘Anha), sio tu kwamba alikuwa ni wa kupigiwa mfano kwa wanawake (walioolewa) na kina mama, lakini alikuwa ni mfafanuzi wa Qur-aan, mwenye mamlaka katika Hadiyth na mwenye ujuzi katika Shari’ah ya Kiislamu. Amesimulia sio chini ya ahaadiyth 2,210 ambazo zinawapa Waislamu uoni wa ndani ulio umuhimu kwenye Maisha ya Mwisho ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na tabia zake, hivyo amehifadhi Sunnah ya Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
- Kwa wakati huo, ndoa hii ilifuta ile dhana kwamba mtu hawezi kumuoa binti ya mtu aliyetangaza kuwa ni “ndugu” yake (hata ndani ya uoni wa dini). Dhana hii ilifutwa bila ya kuangalia kwamba kila mmoja wao, Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Abuu Bakr (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alitangaza kuwa ni ndugu. Hili linafafanuliwa ndani ya Hadiyth ifuatayo: Amesimulia ‘Ursa: Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimuomba ‘Abuu Bakr (Radhiya Allaahu ‘Anhu) ampatie mkono wa ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘Anha) kwa ndoa. Abuu Bakr (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alisema: “Lakini mimi ni ndugu yako.” Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akamwambia, “Wewe ni ndugu yangu kwenye dini ya Mungu na Kitabu Chake, lakini yeye (‘Aaishah) ni halali kwangu kumuoa.” (Swahiyh al-Bukhaariy, Juzuu ya 7, Kitabu cha 62, Rakimu 18).
- Ndoa hiyo iliondosha (imani ya) sihiri ya mapagani wa Kiarabu kwamba ni kisirani kuoana ndani ya mwezi wa Shawwaal. Walifikiria kwamba mwezi huo umebeba ishara hii mbaya kwani neno Shawwaal limetokana na Shaala, ambalo jina lenyewe liliaminika kuchukua ukuba. Hadiyth Swahiyh inaonesha kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘Anha) walioana ndani ya mwezi huu.
HUKO NYUMA HAIKUWA NI YENYE KUSUMBUA
Hapo juu, tumeonesha ukweli kwamba ndoa wakati wa baleghe ilikuwa ni tendo linalokubaliwa baina ya “tamaduni za kale” za wakati huu, lakini mahsusi baina ya Washemi wa Mashariki ya Kati (yaani Wayahudi, Waarabu, n.k.). Kwa kuongezea ushahidi wa ndoa ya Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘Anha) haikuwa kiini cha mazungumzo kwa wakati huo, hapa chini nawasilisha nukuu kutoka kwa wanawake wawili wa Kimagharibi ambao wameusoma Uislamu kwa kina:
“Haikuwa wazi haswa ni lini ndoa hiyo ilifanyika. Kwa mujibu wa baadhi ya matoleo, ilikuwa ni ndani ya mwezi wa Shawwaal wa Mwaka wa Kwanza, hivyo ni; takribani miezi saba au minane baada ya kufika Madiynah; lakini, kwa mujibu wa wengine, haikufanyika ndoa hiyo hadi baada ya Vita vya Badr, hivyo ni, ndani ya mwezi wa Shawwaal wa mwaka wa pili wa Hijrah. Hakuna toleo lolote linalotoa maoni katika hitilafu ya miaka baina ya Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘Anha) au umri mbichi wa bi harusi ambaye, kwa uhakika, inawezekana hakuwa zaidi ya miaka kumi na ambaye bado alikuwa ameshughulishwa na michezo yake ya kitoto.”[10]
Ndani ya nukuu ya hapo juu, vyanzo vilivyotolewa kuwa (alikuwa na) umri wa zaidi ya miaka tisa ni ‘Nawawiy” na 'Twabariy' Maimamu wote hao wawili an-Nawawiy na 'At-Twabariy' walikuwa ni wanazuoni muhimu wa Kiislamu, lakini kazi zao zina vitu ambavyo ni vyenye usahihi mdogo kwa mujibu wa viwango vya Kiislamu, ambavyo bila ya shaka ndio sababu ya kuhoji ni tarehe gani ilikuwa ni sahihi. Hapa hakuna nukta muhimu yoyote, kwani tumeshakwisha onesha kwamba vyanzo sahihi vya Kiislamu vinaeleza kuwa ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘Anha), alikuwa na “umri wa miaka tisa.” Nukta muhimu ya kuiweka kichwani ni kwamba “hakuna toleo” linalotoa maoni kuhusu tofauti yao ya umri au kwa umri mchanga wa ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘Anha). Kwanini? Kwa sababu ndoa ya mapema kama hiyo ilikuwa ni ya kawaida ndani ya jamii zote za Kishemi – kama zile za Ibraahiym, Muusa, ‘Iysaa na aliyokulia nayo Muhammad (‘Alayhim swalaatuLlaahi was-salaamuh ajma’iyn)!
Mwandishi mwengine ni, Karen Armstrong, huyu alikuwa na nyongeza hii: “Twabariy anasema kwamba alikuwa ni mdogo kwani akiishi nyumbani kwa wazazi wake na ndoa ilitimizwa hapo baadaye alipotimu baleghe”.[11] Hii halikadhalika inaweka wazi kwamba ndoa hiyo ilitimu wakati wa baleghe, na kwamba, haikuwa ni kiini cha mazungumzo. “Twabariy” hapa, itambulike kuwa inamtambulisha Abuu Ja’afar Muhammad bin Jariyr at-Twabariy (225-310 AH / 839-923 CE), ambaye alikuwa ni mwanazuoni mkubwa wa Kiislamu anayetambulika Magharibi kwa fafanuzi zake za Qur-aan na taariykh ya dunia.
Hakuna mshangao wowote wa waandishi hao juu kukubali ukweli kwamba ndoa hiyo ya ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘Anha) na Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ilifanyika pale “Aaishah (Radhiya Allaahu ‘Anha) alipofikia baleghe na kwamba lilikuwa ni jambo la kawaida kwa wakati huo. Hili lisilete mshangao, kwani yeyote anayesoma vyanzo vya Waislamu na tamaduni za Kishemi atalazimika kufikia maamuzi hayo, kwani ni ukweli ulio wazi wa kihistoria. Ni lazima itambulike kwamba waandishi hao wawili wa kike walionukuliwa hawaachi kuufafanua vibaya Uislamu ndani ya maandiko yao (kwa kukusudia au bila ya kukusudia). Inatosha kusema kwamba; kama kutakuwa na habari nyengine yoyote ya “kubomoa”, hawataacha kuiweka wazi. Nabia Abbott, ambaye amefanya chunguzi zenye maana kwenye Uislamu ndani ya maeneo kadhaa, hakika ni mwenye elimu ya nchi za mashariki “Orientalist” kwa upande wa aliye bora kabisa. Kitabu chake ambacho kimenukuliwa hapo juu, ‘Aaishah-The Beloved of Mohammed – ‘Aaishah-Kipenzi cha Muhammad, hakika si chochote zaidi ya kuagua kwa mara ya pili kunakochukiza kwa maisha ya ‘Aaishah (Radhiya Allaahu ‘Anha). Kama kitabu chenye mchanganyo kama huo wa kubahatisha na vyanzo visivyo sahihi vimeandikwa kuhusu mtu mwenye umaarufu ndani ya Magharibi, bila ya shaka hakitakuwa kimebaki katika orodha ya makabati ya wanazuoni. Ni jambo linalotambulika kwamba Watu wenye maarifa ya elimu ya Mashariki wakiwa na kitu cha kuokota kwenye Uislamu, wanapendelea kutoa uamuzi kwenye simulizi iliyo sahihi wakiegemea katika dhana zao zenye kuchora mambo ya kale. Kama simulizi isiyo sahihi itamshushia heshima Mtume wetu mpenzi Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), itakuwa ni yenye kunukuliwa kila mara. Hata hivyo, kitu chochote kilicho sahihi ambacho kinaendana kinyume na dhana zao, kinakataliwa kwa urahisi kabisa. Ni sawa na kuandika taariykh ya maisha ya ‘Iysaa na kutumia nukuu kutoka Injili isiyothibitika ili kumdumaza Mtakatifu wa Kikristo wakati wowote inapoonekana sawa kutoa mawazo yenye kinyongo. Hivi ndivyo ambavyo Wataalamu wa elimu ya Mashariki na wamishionari wa Kikristo wanavyomfaya Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa karne. Kwa wale wanaotaka kuelewa zaidi kuhusu hili, tafadhali soma makala yetu Orientalism, Misinformation and Islam – Utaalamu wa elimu ya Mashariki, Upotoshaji na Uislamu.
[5] Gerald Sigal, The Jew and the Christian Missionary - Mishionari ya Wayahudi na Wakristo, Kimechapishwa na Ktav Publishing House, 1981, uk. 28
[6] “Afrika ya Kati”, The New Encyclopaedia Britannica, Toleo la 15, Juzuu ya 15, uk. 646. Pia angalia “Aboriginal Australia”, The New Encyclopaedia Britannica, Toleo la 15 (1987), Juzuu ya 14, uk. 425. Kwa maelezo zaidi kuhusu ndoa za utamaduni ndani ya Kipindi cha Kibiblia, angalia Israel: Its Life and Culture - Israel: Maisha Yake na Tamaduni Zake, kilichoandikwa na Johannes Pedersen, Juzuu ya 1, uk. 60.
[7] Herman H. Ploss, Max Bartels na Haul Bartels, Woman - Mwanamke, Juzuu ya 1, Kimechapishwa na Lord & Bransby, 1988, uk. 563.
[8] Tafsiri ya Kiingereza ya Swahiyh Muslim, Juzuu ya 2, Kimechapishwa na International Islamic Publishing House, Riyaadh, Saudi Arabia, uk. 715.
[9] Theodor H. Vandevelde, Ideal Marriage: Its Physiology and Technique – Ndoa Yenye Lengo: Fiziolojia yake na Utaalamu Wake, Kimechapishwa na Greenwood Publishind Group, 1980, uk. 243.
[10] Nabia Abbott, ‘Aaishah-The Beloved of Mohammed - ‘Aaishah- Kipenzi cha Muhammad, Kimechapishwa na Vitabu vya As-Saqi, London, 1985,uk. 7.
[11] Karen Armstrong, Muhamamd: A Biography of the Prophet – Muhammad: Maisha ya Mtume, Kimechapishwa na Harpser San Fransico, 1992, uk. 157.