Ndugu wa Radhwaa’ah (Kunyonya Ziwa Moja) Ni Mahram Wangu? Naweza Kukaa Mbele Yake Bila Ya Hijaab?

SWALI:

 

Assalam alaykum warahmatu llah wabarakat shukran sana ndugu zangu wa alhidaya kwa kutusaidia najua ndugu mlonyonya ziwa moja hamfai kuoana je ukikaa kichwa wazi mbele ya ndugu yako huyo si haram.


 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kukaa mbele ya ndugu mlionyonya ukiwa kichwa wazi. Ndugu mlionyonya titi la mama mmoja ni Mahram yako kwa kuwa hamuwezi kuoana kisheria kabisa.

 

Kwa minajili hiyo, Uislamu umefanya sahali maingiliano na pia kivazi mbele ya aliye Mahram yako. Miongoni mwa mambo hayo ni kuruhusika kudhihirisha pambo lako kwa walio Mahram wako. Hata hivyo, haifai kabisa mbele ya Mahram yako kukaa ovyo ovyo bila kudhibiti nidhamu za kivazi. Kwa ajili hiyo vazi linatakiwa kuwa ni la sitara kabisa japokuwa litakuwa masharti yatakuwa chini ya yale anayotakiwa mwanamke ayatimize akiwa anatoka nje. Hayo yanapatikana katika Suratun Nuur (24), Aayah ya 31.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

Share