Anataka Kusilimu Lakini Anataka Kwanza Aonyeshwe Wapi Kwenye Qur-aan Kuna Amri Kumi Za Muusa, Na Kwa Nini Waislam Wanaswali Ijum
SWALI:
Assalam alaikum.kuna rafiki yangu anataka kusilimu. Yeye ni msabato, na amekuwa karibu miezi miwili anajifunza uislamu. Mambo yanayomtatiza anataka aoneshwe wapi kwenye quran wameandika amri kumi alizopewa nabii Musa (as). Na kwa nini waislamu wanasali ijumaa badala ya jumamosi. Naomba mnisaidie majibu
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika jina la Allaah au Mtume, usifupishe mbele yake kwa kuweka (S.W.) au (S.A.W.)
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu amri kumi za Nabii Musa (‘Alayhis Salaam) katika Qur-aan na kuswaliwa Swalah ya Ijumaa.
1. Usiwe na miungu mingine:
2. Usijifanyie sanamu za miungu za kuchonga:
3. Usivisujudie wala kuvitumikia:
Hizi nukta tatu za juu zinahusiana na ushirikina ambao umepigwa vita vikali
a. Amepitisha Mola wako Mlezi usimuabudu ila Yeye (17: 23).
b. Muabuduni Allaah wala msimshirikishe Yeye na chochote (4: 36).
c. Na miongoni mwa watu wapo wenye kuchukua miungu washirika wanaowapenda
d. Na hakika Tumewatuma kwa kila Ummah Mitume, na Tukawaambia: Muabuduni Allaah tu na mjiepushe na Twaaghuuti (anayeabudiwa asiyekuwa Allaah) {16: 36}.
e. Sema: Allaah ni Mmoja tu. Allaah ndiye Mwenye kukusudiwa. Hakuzaa wala Hakuzaliwa na hakuna anayefanana Naye (112: 1-4).
f. Mwenyezi Mungu Hasamehe dhambi ya kushirikishwa (4: 48, 116)
4. Waheshimu baba na mama yako: Kuwaheshimu wazazi imekuja katika Qur-aan baada ya kumuabudu Allaah. Kutowaheshimu wazazi ni katika madhambi makubwa.
a. Anasema Aliyetukuka: Na kuwafanyia wema wazazi. Na wanapofikia uzee mmoja wao au wote wawili, usiwaambie uff (neno ndogo hata kusema ah!) ... na uwaambie maneno mema (17: 23-24).
b. Wafanyie wema wazazi wako (4: 36).
c. Mnishukuru Mimi na wazazi wako. Na wakikulazimisha kunishirikisha kwa usilokuwa nalo elimu usiwatii (wazazi wako) lakini suhubiana nao duniani kwa wema (31: 14 – 15).
5. Usizini: Uzinzi ni dhambi kubwa katika Uislamu kiasi ambacho mwenye kuzini akiwa ameoa au hajaoa au kuolewa ana adhabu kali. Mwenyezi Mungu anatuamuru hata tusije karibu na zinaa (17: 32).
6. Usiue: Kuua pia ni katika madhambi makubwa ambayo anapata adhabu mwenye kufanya kitendo hicho. Mwenyezi Mungu Asema kuwa yeyote mwenye kuua nafsi moja ni kama ambavyo ameua walimwengu wote na kuhuisha nafsi moja ni
7. Usiibe: Kuiba ni katika dhambi kubwa na mwenye kufanya
8. Usimshuhudie jirani yako uongo: Jirani ni mtu muhimu katika jamii. Uislamu umehimiza
9. Usimtamani mke wa jirani yako wala vitu vyake: Kufanya hivyo ni kutoka katika ujirani mwema na kuvunja ujirani mwema. Maelezo tayari tumeyaandika hapo juu. Na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Na kumwekea mshirika wakati Yeye ndiye Aliyekuumba, kumuua mwanao ili asile nawe na kuzini na mke wa jirani yako” (al-Bukhaariy, Muslim na an-Nasaa’iy).
10. Adhimisha siku ya Sabato: Sabato ya Waislamu ni siku ya Ijumaa wala sio Jumamosi. Hiyo ni kuwa siku ya Ijumaa ni siku bora na tukufu hapa duniani. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Siku bora iliyochomoza jua ni Ijumaa, kwani ndani yake aliumbwa Aadam (‘Alayhis salaam) na siku hiyo aliingizwa Peponi na kwayo alitolewa, na Qiyaamah hakitasimama ila Ijumaa” (Muslim). Siku hii ni sikukuu ya Waislamu ulimwenguni. Hiyo ni siku ambayo inafaa kwa Muislamu kuiheshimu, hivyo kwenda Msikitini mapema na kufanya Ibadah. Japokuwa sikukuu kwa Muislamu anaruhusiwa kufanya kazi kabla ya Ibadah hiyo mahsusi au baada yake. Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Anasema: “Na itakapokwisha Swalah, tawanyikeni katika ardhi mtafute fadhila za Allaah, na mkumbukeni Allaah kwa wingi ili mpate kufaulu” (62: 10).
Ama kuhusu kipengele cha pili cha swali lako kuhusu kwa nini Waislamu huswali Ijumaa, ni kuwa sisi Waislamu tunaswali siku ya Ijumaa badala ya Jumamosi kwa kuwa tumeagiziwa
“Enyi Mlioamini! Kukiadhiniwa kwa ajili ya Swalah ya Ijumaa, nendeni upesi kumtaja Allaah na acheni biashara. Kufanya hivi ni bora kwenu ikiwa mnajua” (62: 9).
Na Allaah Anajua zaidi