Mtu Aliyepotelewa Na Akili Kujiua Nini Hukmu Yake?

 

Mtu Aliyepotelewa Na Akili Kujiua Nini Hukmu Yake?

 

Alhidaaya.com

 

 

 

 

SWALI:

 

Assalamu aleykum, nini hatima ya mtu aliyejidhuru na kufikia kuutoa uhai wake kama kunywa sumu au kujinyonga baada ya kufikwa na maradhi ya wasiwasi/ kubadilikwa na akili kwa muda au nusu wazimu, yaani katika akili yake timamu mtu hawezi kufanya jambo hilo na alikuwa mcha Mungu hapo awali. Wabillahi Tawfiq........

 

 

 

JIBU:

 

 

 

AlhamduliLLaah Himidi Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa) Rabb wa walimwengu, Swalaah na Salaam zimshukie Nabiy Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhwiya Allaahu 'anhum) na waliowafuata kwa wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

 

Ikiwa amepoteza akili kabisa, akijitoa maisha yake hatakuwa na lawama yoyote mbele ya Allaah Aliyetukuka, kwani sheria inamchukulia mwenye akili kwa kumzawadia au kumuadhibu. Pindi mtu anapokosa akili kalamu hunyanyuliwa juu yake mpaka atakapopata akili au akarudi katika hali yake ya kawaida.

 

Ama ikiwa anapoteza akili na mara nyingine inarudi itategemea amejiua wakati gani. Lau atajiua wakati akili imerudi kuwa timamu atakuwa amekufa katika ukafiri. Na ikiwa atajiua wakati ambao amepoteza akili hukumu yake itakuwa kama maelezo yaliyo juu.

 

Ama mtu akiwa na wasiwasi huhesabiwa akili yake ni timamu kabisa na sheria inamchukulia kama mtu wa kawaida. Hivyo, akijiua atakuwa amekufa katika ukafiri na makazi yake yatakuwa Motoni kulinga na vile alivyojiua kama inavyotaja katika Hadiyth:

 

Anasema Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kutoka katika Hadiyth iliyosimuliwa na Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu)

 

((مَنْ تَرَدَّى مِنْ جَبَلٍ فَقَتَلَ نَفْسَهُ، فَهْوَ فِي نَارِ جَهَنَّمَ، يَتَرَدَّى فِيهِ خَالِدًا مُخَلَّدًا فِيهَا أَبَدًا، وَمَنْ تَحَسَّى سَمًّا فَقَتَلَ نَفْسَهُ، فَسَمُّهُ فِي يَدِهِ، يَتَحَسَّاهُ فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَالِدًا مُخَلَّدًا فِيهَا أَبَدًا، وَمَنْ قَتَلَ نَفْسَهُ بِحَدِيدَةٍ، فَحَدِيدَتُهُ فِي يَدِهِ، يَجَأُ بِهَا فِي بَطْنِهِ فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَالِدًا مُخَلَّدًا فِيهَا أَبَدًا)) البخاري ومسلم

 ((Yeyote atakayejitupa kutoka mlimani na kujiua, atatupwa ndani ya moto milele. Atakayekunywa sumu na kujiua, basi atatupwa motoni na huko atakuwa akiinywa hiyo sumu milele. Atakayejiua kwa kipande cha chuma, atatiwa motoni akiwa na kipande hicho cha chuma akijitwanga nacho tumboni kwake humo motoni milele))].  [Al-Bukhaariy na Muslim]

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share