Mtoto Aliyezaliwa Nje Ya Ndoa Vipi Anaweza Kutambulishwa Na Ataandikishwaje Kwenye Cheti

SWALI:

 

SUALA LANGU LINAULIZA VIPI ANAWEZA KUOLEWA MTOTO WA ZINAA WARKA WA NDOA PAMOJA NA WALIO HUDHURIA KATIKA MALKA WATAJUULISHWA NI BINTI WA NANI SHUKRAN NDUGU YENU HILAL

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu ndoa ya mtoto wa nje ya ndoa.

Ni nasaha yetu kwa kila mmoja wetu ajiepushe sana na zinaa kwa njia zote ambazo zimewekwa na sheria. Ikiwa tutafanya hivyo basi hatutakuwa na shida ya kuuliza ni jina gani atumie mtoto aliyezaliwa nje ya ndoa kwani kila mmoja atakuwa amezaliwa ndani ya ndoa halali.

 

Ama ikiwa imetokea kuwa mtoto amezaliwa nje ya ndoa basi yeye hana makosa bali makosa makubwa ni kwa mwanamme na mwanamke waliofanya dhambi kubwa hilo katika muono wa Kiislamu. Hivyo, ni muhimu waliozini watake msamaha wa Allaah Aliyetukuka kwa kutimiza masharti yafuatayo. Nayo ni:

 

  1. Kujuta kwa kufanya kosa hilo.

  2. Kuazimia kutorudia tena kosa hilo.

  3. Kuacha kosa hilo.

  4. Kufanya mema mengi.

 

Tukija katika swali lako ni kuwa ikiwa kosa hilo tayari limefanywa mtoto huyo anaweza kuitwa kwa ubini wa mamake au kwa ubini wa ‘Abdullaah. Mfano ikiwa mtoto ni msichana basi ataitwa Faatwimah bint Laylaa au Faatwimah bint ‘Abdillaah kwani sote ni waja wa Allaah Aliyetukuka.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share