Supu Ya Adesi Na Brokoli
Supu Ya Adesi Na Brokoli
Vipimo
Adesi - 1 Kikombe cha chai
Brokoli - 1 Msongo
Viazi - 2
Kitunguu - 1 Kikubwa
Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 1 Kijiko cha chai
Karoti - 2
Nyanya - 1
Parsley - ¼ Kikombe
Pilipili manga - 1 Kijiko cha chai
Chumvi - Kiasi
Kidonge cha supu - 1
Ndimu - 1 Kijiko cha supu
Mafuta ya zaytuni - Kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Osha adesi na chemsha hadi iive.
- Katakata karoti, viazi, brokoli, nyanya na vitunguu.
- Kisha chemsha pamoja karoti, brokoli na viazi hadi ziwive.
- Tia mafuta katika sufuria na ukaange vitunguu mpaka vilainike, tia thomu, kisha nyanya na endelea kukaanga.
- Halafu tia pilipili manga, kidonge cha supu na chumvi.
- Kisha mimina vile vitu ulivyochemsha pamoja na supu yake katika mkaango.
- Tia vitu vyote katika mashine ya kusagia.
- Tia parsley na usage kidogo tu.
- Kisha rudisha katika sufuria kwenye moto, tia ndimu na ipike kidogo kwa muda wa dakika moja tu na itakuwa tayari kwa kuliwa.