009-Hakimu Wa Kiislamu: Sura Ya Tatu
SURA YA TATU
HATI
Nyaraka
Mara nyengine, hati za karatasi zinakubaliwa
Ndani ya Sheria ya Ushahidi inaruhusu hati kuwasilishwa Mahkamani kama ni sehemu ya ushahidi. Hati hizi zipo za aina mbili. Aina ya kwanza ni zile za msingi (primary) ambazo ni za asili na aina ya pili ni zile ambazo zinathibitisha kuwepo hiyo aina ya kwanza (secondary). Kwa mfano nakala ya cheti cha ndoa inaweza kuwa ni ithbati kwamba kipo cheti halisi cha ndoa. Hivyo, nakala kwa hapa ni aina ya pili na kile cheti halisi ndio aina ya kwanza.[2] Pia maelezo ya mdomo juu ya kuthibitisha ukweli wa hati unatambulika kuangukia aina ya pili ya ushahidi wa hati.[3] Hakuna hati inayoruhusiwa kuthibitishwa Mahkamani isipokuwa pale yatakapotolewa maelezo ya shahidi.[4]
Wito Kwa Mdaiwa
Ni lazima Mahkama itoe wito kwa mdai pale taratibu za kufungua kesi zinapokamilika. Hata hivyo, wanachuoni hawakutoa maelezo ya kina kuhusiana na utoaji wa wito kwa mdai, isipokuwa Ibn Qudaamah na al-Khassaaf.[5]
Utaratibu wa wito wa kufika Mahkamani kwa mdaiwa unajulikana kwa al-Adwa wa l-l’adu (Bidii ya kumtafuta mdaiwa) na kuegemezwa hoja hiyo kwa Abu Yuusuf, ambaye ameeleza kwamba pale kesi inapofunguliwa Mahkamani na mdaiwa kutambuliwa kuwa anaishi mji huo huo, wito huo utapelekwa pamoja na aliyefungua kesi na tarishi ambao watamleta mdaiwa yeye binafsi au wakala wake.
Kwa mujibu wa Abu Yuusuf, utaratibu wa al-‘Adwa wa l-l’ada una msingi kutoka Istihsaan[6] na sio Qiyaas[7], na Maswahaba walifanya hivyo na hakuna aliyeukataa.[8]
Azad anaendelea kusema kwamba; inapotokea kuwa mdaiwa anaishi nje ya mji, kwa usafiri wa siku nzima. Hakimu ataandika ushahidi uliotolewa na mdai na kisha kumpelekea mdaiwa, akimpa amri ya kufika na kujibu madai. Kwa mujibu wa Ibn Qudaamah na al-Khassaf, maelezo hayo yanatolewa kutoka kwenye maamuzi precedence tofauti yaliyotolewa kutoka kwa Makhalifa waongofu.
Kwa mujibu wa kifungu 20 cha Sheria ya Mwenendo wa Madai ya
Wito wowote unaopelekwa kwa mdaiwa kumtaka afike Mahkamani ni lazima uwe na ithibati kwamba umetoka Mahkamani na ni amri ya Hakimu. Hivyo, wito huo uwe na ushahidi wa Hakimu (mfano saini) na nembo ya Mahkama ukipelekwa na tarishi.
Itakapotokezea mdaiwa kutoweza kufika kwa sababu za msingi
Imaam ash-Shafi’iy anakubaliana na Hakimu kuhamia kwenye eneo la mdaiwa ikiwa anayedaiwa ni mwanamke. Ametumia kisa cha Unays aliyeamrishwa na Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
“Nenda ewe Unays kwa mwanamke wa (kesi hii) hili, akikubali (tuhuma za zinaa nje ya ndoa), mpige mawe hadi kufa.”[12]
Sheria ya Mwenendo wa Madai inaeleza
Kutotii Kwa Mdaiwa Na Kuvamia Eneo La Mdaiwa
Mdaiwa atawajibika kuadhibiwa kwa kutofika Mahkamani siku aliyopangiwa kufika ikiwa amepokea na kuukubali wito. Ni kosa la jinai kuidharau Mahkama na atawajibika kuadhibiwa. Hata hivyo, adhabu ya aliyekataa kupokea wito na kutofika ni kubwa kuliko kwa mtu aliyepokea na kukataa kufika[16].
Kama mdaiwa atajificha na kumkimbia tarishi, Hakimu atamuandikia walii kwa lengo la kumfikisha.
Itakapotokezea kutolewa habari kwamba mdaiwa aliwahi kuonekana kwa ushahidi wa mdai na walii ambaye ameshindwa kumfikisha mdaiwa Mahkamani. Na
Lakini kwa mujibu wa al-Mawardi kwenye kesi ya mdaiwa kutotii amri ya kufika Mahkamani. Hakimu anaweza kutumia moja kati ya njia zifuatazo:
1) Kumlazimisha kwa msaada wa tarishi kufika Mahkamani.
2) Kuihamisha kesi yake mamlaka ya juu ambayo itamlazimisha kufika Mahkamani.
3) Kuteua watu wawili waadilifu ambao watamwita mbele ya mlango wa nyumba yake kufika Mahkamani na kujibu madai[17].
Kwa maoni ya Maliki anaeleza kwamba, Hakimu asimlazimishe mdaiwa, isipokuwa
Al-Khassaaf anasema kwamba wanachuoni wetu wanaruhusu kufanya uvamizi kwenye eneo la mdaiwa wa fedha (mwenye deni) ambaye kwa makusudi anajificha. Hakimu Abu Yuusuf ameshawahi kutumia njia hii. Kwa maelezo ya as-Sarkhasi, utaratibu huu haufai.
Mfumo wa kuvamia kwenye kesi kama hii utakuwa
Hakimu atawapeleka watu wawili madhubuti, matarishi, wanawake na wahudumu. Matarishi watasimama kuizunguka nyuma ili
Kwa kutetea hoja hiyo, al-Khassaaf ametoa vigezo vya Makhalifa waongofu, lakini uvamizi waliofanya unahusu maeneo yanayotuhumiwa kwa jinai, kama ulevi na kucheza dansi.
Ikiwa kwa njia hizo zote hazijafanikisha kumleta mdaiwa Mahkamani, Hakimu ataandika ushahidi uliotolewa na mdai na akiukubali ushahidi huo atatoa hukumu ya upande mmoja (bila ya kumsikiliza mdaiwa)[19].
Maelezo yote hapo juu yanaonesha wazi kwamba Mahakimu wa mwanzo wa Kiislamu walikuwa na hadhari kuhusiana na wito na huduma hizo. Ilikuwa ni wajibu wa Mahkama ya mamlaka ya juu kumtaarifu mdaiwa kuhusiana na hatua hiyo ili aweze kufika Mahkamani kujibu madai. Tofautisha na maoni ya Joseph Schacht kama ifuatavyo:
“Shari’ah za Kiislamu bado zinatumia njia za zamani za kuanzisha vitendo, ambavyo vinahusisha mdai kumkamata mdaiwa na kumburuza mbele ya Jaji (Hakimu)”[20].
Sheria inaruhusu kubandikwa hati ya wito kwenye nyumba ya mdaiwa. Njia hii hufuatwa iwapo Mahkama imeamini kwamba mdaiwa anakwepa kupatiwa wito huo au iwapo hapatikani kabisa au ameshindwa yeye binafsi au wakala wake kupokea wito huo.[21]Iwapo mpeleka notisi ametumia taratibu ya kuibandika hati ya wito, atatakiwa kula kiapo au Mahkama inaweza kumuamuru kwenda Mahkama nyengine ili kuthibitisha maelezo yake.[22]
Mahkama inaweza kuamuru mambo yafuatayo juu ya mtu ambaye amepatiwa hati ya wito na ameshindwa kufuata amri ya kufika:
a) Kutoa hati ya kukamatwa (arrest warrant)
b) Kushikilia na kuiuza
c) Kumtoza faini
d) Kuamuru kuwasilisha dhamana ya
Kufika Mdaiwa Mahkamani
Pale madai yatakapotolewa na kukamilisha taratibu
Kila dai linalofunguliwa mbele ya Hakimu, ni lazima lifuate taratibu maalum za Sheria. Dai lililofuata taratibu za Sheria katika ufunguzi wake, itamlazimu mdaiwa kufika mbele ya Hakimu kujibu madai. [25]
Majibu Kwa Njia Ya Kujitoa
Pale wadaawa wanapofika Mahkamani, mdai ataulizwa kueleza kesi yake na
Pale mdaiwa anapobisha dai
Sheria inaeleza kwamba, mdaiwa atahitajika kuwasilisha majibu ya madai siku ya mwanzo ya kusikilizwa kesi yake au pale Mahkama itakapoamuru vyenginevyo.[27]
Mdaiwa katika kesi anaweza kujitoa dhidi ya madai ya mdai, kwa msingi wa kudai haki au dai. Kujitoa kwake hakutakuwa na ulazima kwamba iwe ni kwa misingi ya kulipwa au kutolipwa haki yake. Kujitoa huku kutakuwa na nguvu
Iwapo kujitoa kwa mdaiwa kumezuiliwa na Mahkama au haiwezekani kwa mujibu wa hati ya mdai, mdaiwa atatakiwa kufungua dai jengine jipya kwa ajili ya kujitoa.
Iwapo imethibiti kwamba dai la kujitoa kwa mdaiwa ni la msingi, Mahkama inaweza kutoa amri ya kumvua mdaiwa dhidi ya madai ya mdai. Mahkama pia inaweza kuamuru malipo yoyote kutoka kwa mdai kwenda kwa mdaiwa.[28]
[1] Fataawa ‘Alamgiri, Juzuu ya III, uk. 584; al-Majallah, uk. 297; pia angalia Sheria ya Ushahidi ya Daftari la Benki, Sura ya 6, S. 3 – 6.
[2] Sheria ya Ushahidi, S. cha 63
[3] Sheria ya Ushahidi, S. 63 (e)
[4] Sheria ya Ushahidi, S. 67
[5] Azad, Judicial System of Islam, uk. 80.
[6] Twaha Jaabir al-Alwany katika kitabu cha Uswuulul al-Fiqh ametafsiri Al Istihsaan: Kuikubali Qiyaas-kufananisha ambayo inaonekana kuwa juu kisheria kwa kulinganisha na mfananisho ulio dhahiri. Ni katika maelezo hayo ambapo al Istihsaan inakuja kwa mara kadhaa kutafsiriwa kama ni “Hiari ya Mwanachuoni”.
[7] Qiyaas: inahusu suala kwa kulifananisha na jengine, pia suala hilo linazungumzwa ndani ya Qur-aan au Sunnah.
[8] Azad, Judicial System of Islam, uk. 81.
[9] Sheria ya Mwenendo wa Madai, O. V, r. 1 (2) na (3).
[10] Sheria ya Mwenendo wa Madai, O. V, r. 16.
[11] Ibid, O. V, r. 17.
[12] Azad, Judicial System of Islam, uk. 83.
[13] Sheria ya Mwenendo wa Madai, O. V, r. 10; angalia pia Sheria ya Mahkama ya Ardhi no. 12 ya 1994, S. 23 – 25.
[14] Sheria ya Mwenendo wa Madai, O. V, r. 18.
[15] Sheria ya Mwenendo wa Madai, S. 111 (1).
[16] Azad, Judicial System of Islam, uk. 82.
[17] Azad, Judicial System of Islam, uk. 83.
[18] Azad, Judicial System of Islam, uk. 83.
[19] Ibn Qudamah; Akhbaar al-Qudhaat, IX, uk. 109.
[20] An Introduction to Islamic Law, uk. 16.
[21] Sheria ya Mwenendo wa madai, O. V, r. 17 na 20.
[22] Sheria ya Mwenendo wa Madai, O. V, r. 19.
[23] Sheria ya Mwenendo wa Madai, S. 24.
[24] Sheria ya Mwenendo wa Madai, O. VII, r. 12.
[25] Sheria ya Mwenendo wa Madai, S. 19 na 20.
[26] Durru’l-Mukhtaar’, Juzuu ya IV, uk. 391, pia Raddu’l-Mukhtaar.
[27] Sheria ya Mwenendo wa Madai, O. VIII, r. 1.
[28] Sheria ya Mwenendo wa Madai, O. VIII, r. 6 (1) na (8).