010-Hakimu Wa Kiislamu: Sura Ya Nne
SURA YA NNE
KUSIKILIZA KESI
Sehemu Ya Mahkama
Sehemu yoyote inaweza kutangazwa
Kwa upande mwengine, Sheria inaeleza kwamba ni lazima kesi isikilizwe kwenye Mahkama ya wazi[2] isipokuwa pale Mahkama inaporidhika ya kwamba haitotenda haki iwapo kesi itasikilizwa humo.[3] Hivyo, Mahkama itakuwa na uwezo wa kusiliza kesi sehemu nyengine yoyote baada ya kuweka kumbukumbu za hoja na sababu ya kutosililiza kesi hiyo Mahkama ya wazi.
Hamna Hukumu Bila Ya Kusikilizwa
Lengo kuu la hapa ni kuwapa haki ya kusikilizwa pande zote mbili za kesi (mdai na mdaiwa) ili kuondosha hukumu itakayotolewa kwa maelezo ya upande mmoja. Kanuni hii imechukuliwa kutoka Hadiyth iliyotolewa na ‘Aliy bin Abii Twaalib (Radhiya Allaahu ‘Anhu) alipopatiwa muongozo kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kwa mnasaba wa uteuzi wake nchini Yemen kushikilia mamlaka ya kutoa hukumu:
Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) alimpeleka (Sayyidna ‘Aliy)
Sheria inaeleza kwamba hakuna ruhusa ya kutoa hukumu kwa upande mmoja hadi pale hati ya taarifa inapotolewa kwa upande ulioshindwa kuhudhuria. Hii itampa nafasi kwa mara nyengine kuhudhuria Mahkamani.[5]
Hukumu Dhidi Ya Upande Mmoja - Al-Qadhaa ‘Alaa al-Ghaib
Ibn Qudaamah ambaye ni mwanachuoni wa Hanbali ana maelezo ya kwamba hukumu kuhusiana na haki za wanaadamu zaweza kutolewa dhidi ya aliyeshindwa kuhudhuria Mahkamani. Ametumia Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam):
Hind alisema: “Ewe Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) Abu Sufyaan ni mtu bakhili na hanipatii kitakachonitosheleza mimi na watoto wangu” Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: “Chukua kitakachokutosheleza wewe na mtoto wako wa kiume kulingana na mahitaji (yenu).”[6]
Pia Qudaamah anaeleza kwamba; hukumu ambayo imetolewa ya upande mmoja na bila ya kumpatia nafasi ya kumsikiliza mdaiwa iwekwe pembeni ikiwa tu,
Ibn Qudaamah pia anaeleza kwamba, kwa mujibu wa wanachuoni walio wengi kuwa, hukumu iliyotolewa upande mmoja sio sahihi ikiwa mdaiwa yupo ndani ya mji.[7]
Hadiyth aliyotumia Ibn Qudaamah sio amri ya kisheria iliyotolewa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam). Ni kipande cha ushauri wa Kishari’ah na maelezo ya dini ili kuwapatia Waislamu muongozo kuhusiana na wale ambao hawapo tayari kufika Mahkamani kutoa ushahidi wao kwa kuegemea sababu zisizo msingi. Maelezo ya Ibn Qudaamah yanakataliwa kwa kutumia Hadiyth ifuatayo:
Ibn ‘Abbaas amesimulia kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kama watu watapewa kulingana na misingi ya madai
Kwa upande wa madhehebu ya Hanafi, mwanachuoni wa Kihanafi aitwae Al-Marghinani anakubali kwamba hukumu ya upande mmoja sio sahihi isipokuwa iwe mbele ya wakala wa yule asiyehudhuria.[9] Ibn Farhaan na Maaliki wote wanakubali mawazo ya Ibn Qudaamah.[10]
Al-Mawardi ametenga kurasa kadhaa kuhusiana na hili na kutoa mjadala mrefu chini ya mada inayoitwa Al-Qadhaa ‘Alaa al-Ghaib – Hukumu Dhidi ya asiyekuwepo. Al-Mawardi ambaye anafuata misimamo ya ash-Shafi’iy, ana mawazo ya kwamba hukumu dhidi ya mtu asiyekuwepo Mahkamani ni sahihi, ikiwa ni kwa qadhiya ya
Kwa Maalik, hukumu kama hiyo ni sahihi katika
Hukumu dhidi ya asiyekuwepo Mahkamani lakini yupo ndani ya mji sio sahihi kwa mafundisho ya ash-Shafi’iy. Lakini hukumu hiyo hiyo ni sahihi kwa mujibu wa Ibn Shubrumah, Ahmad na Is-haaq kama ilivyotolewa maelezo na Al-Mawardi bin Shubrumah ambaye amesema kwa mujibu wa al-Mawardi: “Nitatoa hukumu dhidi ya mtu aliyekuwa nyuma ya ukuta mwengine na ambaye hayupo mbele yangu.”[13]
Al-Mawardi baada ya kutoa maelezo ya wanachuoni wakubwa wakubwa, amekubaliana na mawazo ya ash-Shafi’iy kwamba;
Azad ambaye ni mwanachuoni wa Kihanafi ameeleza kwamba pande zote ni lazima ziwepo Mahkamani. Amenukuu kwa kuikataa hoja za watu wa ash-Shafi’iy kwa kutumia Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ya kwamba walikwenda watu wawili kufanya ahadi mbele ya Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ili kutimiza malengo
Azad anaendelea kutoa hoja kuwa mawazo ya al-Mawardi hayakubaliki kwa karne ya leo. Kwani kipindi cha wanachuoni wa mwanzo, msafara wa mji mmoja kwenda mwengine ulikuwa ni mgumu. Hivyo wanachuoni wakaegemea kwa hukumu kwa aliye mbali (qadhaa ‘ala al-ghaibu) ili kufikia haki. Mahanafi wameingiza na kutumia mwenendo mwengine kwamba pale mdaiwa anaishi kwa muda au maisha yake yote ni maeneo ya mbali na Mahkama, mdai anaruhusika kuiwasilisha kesi yake na kutoa ushahidi na kuangalia kwa makini kuhusiana na ukweli wa ushahidi, atapeleka kumbukumbu za ushahidi wa kesi kwa Hakimu ambaye huyo mdaiwa anaishi.[15]
Azad anamaliza kwa kusema kuwa hukumu ya upande mmoja (
Sheria kwa upande wake inaeleza kuwa pale ambapo mdai amefika Mahkamani lakini mdaiwa hakufika, Mahkama inaweza kuendelea na kesi kwa kumsikiliza mdai na kutolea uamuzi wa upande mmoja iwapo tu mdaiwa alipata wito wa kumuita Mahkamani. Ikiwa haikuthibiti kwamba hati ya wito ilipelekwa, Mahkama itaamuru kutolewa kwa hati ya pili ya kumuita mdai. Mahkama pia inaweza kuakhirisha kesi iwapo mdaiwa hakupatiwa muda muafaka wa taarifa ya kufika Mahkamani.[17]
Iwapo Mahkama imetoa amri ya kusikilizwa upande mmoja, mdaiwa anaweza kupinga hukumu hiyo[18] au kutoa sababu ya msingi ya kutohudhuria kwake na Mahkama ikamuamuru kusikilizwa kesi yake kana kwamba alikuwepo siku ya mwanzo.[19]
Mdai anaposhindwa kufika Mahkamani lakini mdaiwa amefika, Mahkama inaweza kulifuta dai lake (mdai) na hataruhusiwa kufungua dai jengine jipya kama
Kwa upande wa kesi yenye mdai au mdaiwa zaidi ya mmoja, na baadhi
Mdaiwa Kukataa Kujibu
Wanachuoni wa Hanafi wanasema kwamba pale mdaiwa anapoitwa na kuukubali wito wa kufika Mahkamani, lakini akakataa kuzungumza mbele ya Mahkama (kudharau) na kukataa kujibu madai ya mdai, Hakimu atampeleka jela mpaka pale atakapokuwa tayari kujibu madai ya mdai. Ama wanachuoni wa Kishafi’iy kwa mujibu wa al-Mawardi, wanasema kwamba mdaiwa hatofungwa, lakini hukumu itatolewa dhidi yake.
Utaratibu wa kutolea hukumu dhidi ya anayeshindwa kuwasilisha majibu ya madai unaenda sambamba ndani ya Sheria. Kwani mdaiwa anaposhindwa kuyawasilisha majibu yake ndani ya muda aliopatiwa, Mahkama itatoa amri kwa upande mmoja.[23]
Kukubaliana Na Madai (Admission)
Kwa ujumla, Mahkama inakubali mdaiwa kukariri madai (kukubali ukweli wa mdai) bila ya kuhitaji ushahidi mwengine kutoka kwa mdai. Lakini kukubali huko kwa mdaiwa kuwe kumefanywa kwa hiari. Hata kama kumefanywa kwa kutumia nguvu, haitokuwa na nguvu mbele ya Shari'ah. Wala isiwe imefanywa kwa ubishi au mzaha.
Pale mdaiwa anapokubali madai ya mdai na ukweli wake wa mdai, Hakimu atatoa amri ya hukumu itakayompendelea mdai.
Sheria pia inakubaliana na upande wowote kukubali madai ya upande wa pili.[24] Kwa mfano mdaiwa anaweza kukubaliana na madai kwamba alishindwa kulilipa deni la mdai. Baada ya Mahkama kupokea hati inayoonesha upande mmoja kukubaliana na madai ya upande mwengine, Hakimu atatoa hukumu inayoona inafaa.[25]
Kusikiliza Dai
Kanuni zinaweka wazi kuhusiana na kulisikiliza dai. Kanuni muhimu na ya moja kwa moja kwa suala hili ni kwamba dai lazima lisikilizwe mbele ya wadaawa au wawakilishi wao. Mdai,
Hakuna utaratibu wa Mahkama kuteua wakala kusimamia kesi ya yule anayeshindwa kufika Mahkamani kwa upande wa Sheria.
Kuakhirisha Na Kuchelewesha Haki
Aidha, ujio wa kesi ulikuwa ni mchache kwenye kipindi cha wanachuoni wa mwanzo ama kwa sababu nyenginezo, ndio maana hawakusema kitu kuhusiana na kuakhirisha kesi hivyo kuchelewesha katika kutenda uadilifu.
Katika barua ya ‘Umar kwa Abu Muusa (Radhiya Allaahu ‘Anhuma), kama ilivyoelezwa awali, tunaweza kusema kwamba Hakimu atumie akili yake na hekima zake zote katika kesi ambayo ni yenye ujanja na ugumu na anaweza kuakhirisha tamko la hukumu hadi afikie hitimisho lililokuwa sahihi.
Pale ambapo mdai hana mashahidi wake, wanachuoni wamesema kwamba Hakimu anaweza kusubiri mpaka wafike mashahidi mbele yake kwa muda wa siku tatu.[26]
Ama kwa Sheria ni lazima ziwepo sababu za msingi kabla ya kuakhirisha kesi. Kwani haki inayocheleweshwa kutolewa inasababisha haki kukosekana (justice delayed is justice denied). Hata hivyo, Hakimu amepewa nguvu ya kuakhirisha kesi hadi wakati anapoona inafaa. Mahkama inaweza kuakhirisha kuisikiliza kesi mara kwa mara. Katika kila siku inayoikhirishwa kesi, ni lazima Mahkama ipange tarehe nyengine kwa ajili ya pande za kesi kufika kusikiliza kesi
Iwapo muda muwafaka umetolewa na Mahkama, hakutakuwa na ruhusa ya kuakhirisha kesi kwa upande ulioshindwa kuwasilisha ushahidi, au mashahidi au kufanya jambo lolote aliloamrishwa.[28]
Upande wowote utakaoshindwa kujibu masuala yaliyoulizwa, na ambayo Mahkama inaamini anaweza kujibu, Mahkama inaweza kuakhirisha kesi hadi siku nyengine, na kutoa muongozo wa mtu huyo aliyeshindwa kujibu kufika Mahkamani.[29] Iwapo hakufika siku iliyotajwa bila ya sababu ya msingi, Mahkama inaweza kutamka hukumu, au kutoa amri yoyote inayoona inafaa.[30]
[1] Azad, Judicial System In Islam,
[2] Sheria ya Mwenendo wa Madai, O. XXI, r. 5
[3] Sheria ya Mwenendo wa Madai, O. XXX. r. 6.
[4] Al-Bayhaqiy, as-Sunan al-Kubra, X, uk. 137. Pia angalia al-Jami’, I,
[5] Sheria ya Mwenendo wa Madai, O. XI, r. 15.
[6] Al-Mughni, IX,
[7] Al-Mughni, IX,
[8] Muslim, Sahiih.
[9] (a) Al-Murghinani, al-Hidaaya, II,
[10] (a) Ibn Farhuun, Tasbiirah, I,
[11] Al-Mardhi, Adaab al-Qaadhi, II,
[12] Al-Mawardi, Adaab al-Qaadhi, II,
[13] Al-Mawardi, Adaab al-Qaadhi, II,
[14] Azad, Judicial System of Islam,
[15] (a) Azad, Judicial System of Islam,
[16] Azad, Judicial System of Islam,
[17] Sheria ya Mwenendo wa Madai, O. XI, r. 6.
[18] Sheria ya Mwenendo wa Madai, O. XI, r. 14
[19] Sheria ya Mwenendo wa Madai, O. XI, r. 8.
[20] Sheria ya Mwenendo wa Madai, O. XI, r. 9 – 10.
[21] Sheria ya Mwenendo wa Madai, O. XI, r. 11 – 12.
[22] Sheria ya Mwenendo wa Madai, O. XI, r. 13.
[23] Sheria ya Mwenendo wa Madai, O. VIII, r. 10.
[24] Sheria ya Mwenendo wa Madai, O. XIV, r. 1
[25] Sheria ya Mwenendo wa Madai, O. XIV, r. 6.
[26] Kwa mifano, angalia al-Marghinani; al-Hidayah, III, mjadala kuhusiana na Shahadah,
[27] Sheria ya Mwenendo wa Madai, O. XX, r. 1.
[28] Sheria ya Mwenendo wa Madai, O. XX, r. 3.
[29] Sheria ya Mwenendo wa Madai, O. XII, r. 4 (1)
[30] Sheria ya Mwenendo wa Madai, O. XII, r. 4 (2)