Maharage Ya Sosi Ya Nyanya
Maharage Ya Sosi Ya Nyanya
Vipimo
Maharage - 1 Kopo
Kitunguu - 1
Nyanya - 1 Kubwa
Pilipili mbichi- 1-2
Nyanya ya kopo - ½ Kijiko cha chai
Pilipili ya unga - ¼ Kijiko
Chumvi - Kiasi
Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 1 kijiko cha chai
Kidonge cha supu - ½ Kidonge
Mafuta ya zaituni - 4 Vijiko vya supu
Maji - Kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Roweka maharage, kisha chemsha hadi yawive na kulainika; ikiwa unatumia maharage ya mkebe hakikisha unayaosha kwanza.
- Katika sufuria, tia mafuta na kaanga kitunguu na thomu mpaka ibadilike rangi na sio kuungua.
- Kisha tia nyanya (tungule) aina zote mbili, pilipili ya unga na pilipili mbichi, kidonge cha supu na maharage na ufunike na iache katika moto wa kiasi na usikoroge.
- Yakisha kaangika, utayaponda ponda, kisha tia maji ya kiasi na iache itokote kidogo.
- Halafu epua motoni na itakuwa tayari kwa kuliwa na mkate au chapati.