Mchicha Wa Bamia Na Sosi Ya Nyama
Mchicha Wa Bamia Na Sosi Ya Nyama
Vipimo
Mchicha uliokatwa mdogomdogo - 600 gm
Bamia (kata ndogo ndogo) - 2 Vikombe
Nyama ya ng'ombe kata vipande vidogodogo - 2 LB
Kitunguu saumu(thomu/galic) na tangawizi - 1 kijiko cha chai
Pilipili mbichi iliyosagwa (au nyekundu ya unga) - 1 Kijiko cha chai
Vitunguu (kata vidogovidogo) - 3
Nyanya (kata ndogo ndogo) - 3
Nyanya ya kopo - 3 vijiko vya supu
Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 1 kijiko cha supu
Mafuta - ¼ kikombe
Chumvi - kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Chemsha nyama kwa maji ya kiasi, chumvi, thomu na tangawizi, pilipili, na kitunguu kimoja. Hakikisha maji sio mengi ili itakapowiva ibakie supu yake kidogo tu.
- Katika sufuria weka mafuta, kaanga vitunguu mpaka viwe vyekundu kidogo, tia thomu kaanga kidogo tu.
- Tia nyanya kaanga mpaka zilainike, tia nyanya ya kopo.
- Weka mchicha na bamia endelea kukaanga.
- Mimina supu ya nyama, ongeza chumvi ikibidi, iwache kwenye moto kidogo kuwivisha mchicha na bamia..
- Mimina katika bakuli na ikiwa tayari kuliwa.