Mboga Mchanganyiko

Mboga Mchanganyiko

VIPIMO:

Brokoli (Brocoli)  - 1 mche

Karoti - 3

Viazi  - 2

Njegere   (snow-peas)  au zozote - 1 kikombe

Zucchini (kama mamumnya)  -  3

Pililipili mboga za rangi mbali mbali - 1 kila rangi

Mraba ya supu ya nyama - kidonge 1, au supu yenyewe kiasi cha kutia ladha (hakikisha supu isizidi kipimo).

Pilipili manga - 1 kijiko cha chai

Chumvi  - kiasi

Sosi ya soy - 1 kijiko cha supu

Mafuta ya kukaangia  -  1/4 kikombe  

 

NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA 

 

1.Kata kwanza viazi, zuchini na karoti vipande virefu verefu kisha chemsha  kidogo tu. Tia chumvi na        pilipili manga.

2.Tia mafuta katika karai, kaanga vitu vyote  isipokuwa brokoli na mapilipili makubwa.

3. Karibu na kuwiva tia sosi ya soy na kidonge cha supu.

4. Kata au chambua brokoli, kata kata mapilipili na tia katika mchangayiko, ipikike muda wa dakika tano    tu. Changanya vizuri, tayari kuliwa na mkate au wali mweupe. 

 

Kidokezo: 

 

Usikaange au kuchemsha sana mboga  ili usipoteze vitamini zake.

 

 

Share