Viazi Vya Kuoka Vya Kumwagiwa Vitunguu Na Pilipili Boga
Viazi Vya Kuoka Vya Kumwagiwa Vitunguu Na Pilipili Boga
Vipimo
Viazi - 8-10
Kitunguu cha kijani (spring onions) katakakata
Pilipili boga (capsicum) jekundu katakata
Chumvi kiasi
Paprika - 1 kijiko cha chai
Siagi - 1 kijiko cha supu
Mchanganyiko wa sosi ya kijani (kotimiri, pilipili mbichi, methi leaves (majani ya uwatu)
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Saga vitu vya mchanganyiko wa kijani katika blender kwa mafuta kidogo.
- Vioshe viazi vizuri kisha kata kila kiazi vipande na maganda yake.
- Weka viazi katika bakuli la kuokea (Baked) kisha tia paprika na mchanganyiko wa kijani kiasi kijiko 1 cha supu. Tia chumvi changanya vizuri.
- Tia siagi changanya.
- Weka katika oven pika kwa moto wa kiasi 150-180 Deg kwa muda wa saa kasorobo.
- Epua mwagia vitunguu vya kijani na pilipili boga jekundu.
Bis-swihhah wal-hanaa (kula kwa siha na kufurahika)