Mchanganyiko Wa Mboga Za Kuchoma (Baked)
Mchanganyiko Wa Mboga Za Kuchoma (Baked)
Vipimo
Viazi - 5
Karoti - 2
Koliflawa (cauliflower) - ½
Brokoli - 3 misongo (bunch)
Pilipili mboga ya kijani - 1
Pilipili mboga nyekundu - 1
Kitunguu saumu(thomu/galic) iliyosagwa - 1 kijiko cha supu
Pilipili manga iliyosagwa - 1 kijiko cha chai
*Kidonge cha supu (stock) - 1
Parsley kavu iliyokatwa ndogo ndogo (chopped) - 2 vijiko vya supu
Chumvi - kiasi
Mafuta ya zaytuni (olive oil) - 3 vijiko vya supu
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
- Menya viazi katakata vipande vya mchemraba (cubes)
- Katakata karoti vipande virefu virefu vya kiasi
- Katakata mapilipili mboga vipande vya kiasi kiasi
- Chambua koliflawa na brokoli
- Tia mafuta katika karai, kaanga thomu kidogo kisha tia chumvi, pilipili manga, epua weka kando.
- Weka kidonge cha supu katika kibakuli kidogo, tia maji ya moto kiasi vijiko 3 vya supu, koroga kipate kuyayuka iwe supu. Tia katika sufuria uliyokaangakia thomu.
- Weka mboga zote katika bakuli kisha mimina mchanganyiko wa thomu na supu uchanganye vizuri.
- Tia katika treya ya kupikia ndani ya oveni. Zipike mboga (bake) kwa moto wa takriban 350°C kwa muda wa dakika 15-20.
- Epua kisha mwagia parsely na uchanganye kisha mimina katika bakuli la kupakulia ikiwa tayari kuliwa kwa aina za mikate.
* kidonge cha supu ikiwa ni chicken stock au beef stock.