Mboga Ya Zucchini, Bilingani, Viazi Na Mapilipili Mboga
Vipimo
Zucchini (aina ya mumunye) 2
Bilingani 2
Viazi 4
Pilipili boga la kijani 1
Pilipili boga la manjano 1
Pilipili boga jekundu 1
Vitunguu 3
Nyanya 4
Nyanya kopo (tomato paste) 3 vijiko vya supu
Rai ya unga (mustard seeds) 1 kijiko cha chai
Metthi ya unga (uwatu/Funegreek seeds) 1 kijiko cha chai
Pilipili mbichi 2
Pilipili manga ya unga au nyekundu 1 kijiko cha chai
Majani ya mchuzi (curry leaves) 1 Mche
Chumvi kiasi
Mafuta ya kupikia 2 vijko vya supu
Mafuta ya kukaangia mboga kiasi
Namna Ya Kutayarisha Na Kupika
1. Katakata zuchini, bilingani na viazi vipande vikubwa kubwa kiasi, kata viwe na umbo la mraba (cube).
2. Tia mafuta ya kukaangia mboga katika karai uache yashike moto vizuri, kisha kaanga zucchini ziive kidogo utoe na kuzichuja mafuta.
3. Kaanga bilingani hadi zigeuke rangi utoe na uchuje mafuta.
4. Kaanga viazi hadi viive utoea na kuchuja mafuta.
5. Katika karai jengine tia mafuta 2 vijiko vya supu, kaanga vitunguu hadi viwe laini na karibu ya kubadilika rangi.
6. Tia metthi na rai ya unga, majani ya mchuzi (chambua utoe majani pekee) kaanga kidogo tu.
7. Katakata nyanya ndogo ndogo, katakata pilipili mbichi kwa urefu na utie, endelea kukaanga.
8. Tia nyanya ya kopo, pilipili ya unga na chumvi, tia maji
9. Katakata mapilipili boga vipande vikubwa vikubwa uchanganye humo yapikike kwa chini ya dakika moja uepue. (Usiache mapilipili yakavurugika kwa kukaanga
10. Changanya na zucchini, bilingani na viazi, pakuwa katika sahani au bakulia na ikiwa tayari kuliwa kwa aina yoyote ya mkate au wali mweupe.