Mboga Mchanganyiko Na Sosi Ya Uyoga
Mboga Mchanganyiko Na Sosi Ya Uyoga
Vipimo
Viazi - 2
Karoti - 2
Koliflawa (cauliflower) - ¼ ya uwa zima
Brokoli (brocoli) -1 mshikano mdogo (bunch)
Uyoga (mushrooms) - 12-13
Figili mwitu (celery) - 1 mche
Nanaa kavu (dry mint leaves) - 2 vijiko vya supu
Pilipili manga - ½ kijiko cha supu
Kidonge cha supu (stock) - 1
Chumvi - Kiasi
Siagi - 1 kijiko cha supu
Maziwa - 2 vikombe
Namna Ya Kupika Mboga:
- Changanya pamoja katika bakuli, viazi, karoti, koliflawa, brokoli, nusu uyoga, figili mwitu, koleza chumvi kidogo pilipili ukipenda.
- Weka katika bakuli la kupikia ndani ya oven, funika upike (bake) kwa moto wa kiasi hadi mboga ziive. Mboga ziive kiasi tu si mpaka zivurugike.
- Epua weka kando utayarishe sosi ya uyoga.
Namna Ya kupika Sosi Ya Uyoga
- Weka nusu uyoga ulobaki katika mashine ya kusagia (Blender), tia maziwa, kidonge cha supu, pilipili manga, kisha piga ilainike.
- Tia siagi katika kibakuli kidogo weka motoni, mimina sosi uipike kidogo iwe nzito kidogo.
- Changanya na nanaa kavu, pilipili manga kidogo tena, umwagie juu ya mboga uchangaye vizuri.