Mchicha (Swiss Chard) Na Bamia
Mchicha (Swiss Chard) Na Bamia
Vipimo
Majani ya Mchicha (Swiss Chard) - 4 - 5
Bamia - 150 - 250g
Chumvi - 1 kijiko cha chai
Mafuta ya zaituni - ½ kikombe
Maji - 1 gilasi
Kitunguu maji kilokatwakatwa - 1
Namna Ya Kutayraisha Na Kupika
- Katakata sehemu ya juu ya majani ubakishe majani pekee.
- Osha majani kisha katakata kama mchicha wa kawaida .
- Tia mboga katika sufuria, maji na chumvi chemsha kwa dakika 25 hivi.
- Osha bamia uweke tayari ukiwa umezikata vikonyo vyake.
- Mboga ikishachemka kurudia chini mimina bamia, kitunguu, mafuta . Acha ichemke mpaka bamia ziwive ikiwa tayari.
Kidokezo:
Mboga hii ni aina ya mchicha ila hatujui inaitwaje kiswahili, ila tunajua inatiwa Swiss Chard.