Kutumia Huduma Za Wireless Internet Ikiwa Hujui Ni Ya Nani; Je Itakuwa Ni Kumuibia Mtu?
SWALI:
assalam alaykum shehe naanza kwa kuwapongeza kwa kuanzisha hii website inasaidia sana hasa kwa sisi tulio mbali na nchi yetu kwa kuufahamu uislamu vizuri na makini mahala nilipo ni kuna wireless intenet nyingi ila nyingi ni za watu binafsi na zina password ila chache hazina na zingine ni za umma kuzitofautisha kwamba hii ni ya mtu binafsi na hii ni ya umma ni ngumu na hata hivyo wahusikA wa hizi intanet ni vigumu kuwajua je nikitumia kuna makosa? Ni hayo tu waleikum msallaam
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kutumia huduma za wireless internet ikiwa humjui mwenyewe.
Ikiwa zipo wireless nyingi namna hiyo na wewe unaweza kwenda kwa wahusika ukapata ya kwako, kwani kutumia ya mtu mwengine ikiwa unamjua au humjui ni makosa na ni wizi. Sababu ni kuwa wenyewe wanalipia huduma hiyo na ikiwa nawe utaunganisha na kuanza kutumia huduma hiyo utaongeza gharama hata kama ni ndogo, au kuzoretesha huduma yake na kuifanya isiwe na kasi
Hivyo, jiepushe kabisa katika utumiaji wa internet hizo.
Na Allaah Anajua zaidi