Aliyesilimu Akaritadi Anaweza Kurudi Katika Dini Ya Kiislamu?
SWALI:
Mtu aliyesilim kutoka kwenye dini ya kweli kisha baada ya muda fulani akataka kurudi anaruhusiwa?
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho
Mtu ambaye alikuwa ni Muislamu kisha akaritadi anaweza kurudi katika Dini anapoona kuwa amefanya makosa. Na jambo hili lilitokea wakati wa Sayyidna Abu Bakar (Radhiya Allaahu ánhu) ambapo Waarabu waliritadi na baadae wakarudi katika Dini
“Hakika walio amini, kisha wakakufuru, kisha wakaamini, kisha wakazidi ukafiri, Allaah hakuwa wa kuwaghufiria wala wa kuwaongoa njia” (4: 137).