Muislamu Kuwekewa Kiungo Cha Asiyekuwa Muislamu Baada Ya Kufa - Organ Transplant
SWALI:
Assalaamu Aleykum Warahmatul-laahi Ta'ala Wabarakaatuh.
Shukrani zote anastahili Allah (subhanahu wata'ala) mola wa viumbe vyote. Na rehma na amani zimshukie nabii wetu Muhammad (Salla laahu Aleihi Wasallam). Mwanzo kabisa natoa pongezi zangu za dhati kwa maustwaadhi wetu wa alhidaaya na wanachama wote wa hii website kwa kutuma maswali
{A} je transplant ya kubalika katika dini hii yetu ya kiislaam?
{B} je
{C} Na kama yakubalika tena, yafaa muislamu akiwa nahaja
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa maswali yako kuhusu kutoa viungo kwa ajili ya kumsaidia muhitaji.
Hakika ni kuwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ametuusia
Kwa minajili hiyo Uislamu unatazama na kupatia kipaumbele uzima na afya ya mwanaadamu na hata ikafanya ni dharura kwa mwanaadamu kuwa na haki ya kuishi. Kwa hiyo, kukitokea haja ya mtu kufanyiwa transplant basi Uislamu hauna pingamizi bali utakubali
Uislamu hivyo hivyo umemkirimu mwanaadamu akiwa hai na anapokufa pia kwa kiasi ambacho pindi Muislamu anapoaga dunia kuna mambo ambayo anafaa kufanyiwa. Mambo hayo yote ni kwa maslahi ya aliyefariki na kwa kule kukirimiwa hafai kufanyiwa mambo
Hivyo, hakuna tatizo kwa mtu kukubali kwa kutia saini makaratasi kuwa akifa viungo fulani vyake vimsaidie mtu mwengine ambaye ni muhitaji ili kumuokoa na maradhi aliyonayo.
Ama Muislamu kupatiwa kiungo na asiyekuwa Muislamu au kinyume chake yote yakubalika kishari’ah bila ya tatizo lolote lile.
Na Allaah Anajua zaidi