Ndoa Kabla Mtu Hajawa Muislamu, Na Watoto Waliozaliwa Kama Wana Haki Yoyote
SWALI:
Assalam alaikum W.W!
namushukuru Allah baada ya kunipa uwezo wakuuliza shali langu ili nifafanukiwe namuombea amani na rehema za Allah mtume wetu Muhamad S.A.W swala langu ni kuhisu mtu aliye ingia uwislam je kama mtu ameowa na akazaa badae akamini ALLAH na MTIME WAKE na VITABU VYAKE na vyile vyingine vyo vyanapashashwa kuanimi ili uwe muilislam kitu gani anafanya ili ndoa yake iwe halali? Watoto alie zaa mbere yakuamini wana tofauti gani nawele walio zaliwa katika nji ya uzinifu? Sasa kama hamkuunga ndowa mala ya pili kwa mtu huyo ina maana
Wahadh ASS.W.W!
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani kwa swali lako kuhusu ndoa iliyofungwa kabla ya wanandoa kusilimu.
Ama kuhusu swali hili ni kuwa mtu aliyesilimu na mkewe, Uislamu unaikubali ndoa
Hivyo, wanandoa hao hawana haja kufunga ndoa tena ila tu ikiwa wao wenyewe wanaona kufanya hivyo watakuwa na utulivu zaidi.
Na bila shaka watoto waliowazaa kwa ndoa hiyo kabla kusilimu watakuwa wanatambulika
Na Allaah Anajua zaidi