Anaweza Kubadilisha Jina La Baba Wa Mtoto Wake?
SWALI:
ssalaam Aleikum,
Ningependa kuuliza mama aweza kubadilisha jina la baba kwa mtoto wake ambae huyo baba anamkana? kusema kuwa si wake kwa sheria ya dini?
Nna mwenzangu alikuwa na matatizo na mumewe akahama, mume akamfwata kutaka maskizano, bibi akakubali, kwa manufaa ya watoto wawe na maisha ya baba na mama. After a while bibi akawa mzito, akamueleza bwana. akakana kuwa mimba si yake, na hataki kujua, he left. Mtoto akazaliwa, Bibi akajiwachisha kwa kadhi. Bahati mbaya alipofika miezi 6 mtoto akauguwa, kalazwa miezi miwili hospitali, mara atiwa ICU alhamdulillah siku zake ziko akapona. Huyo baba hata kupiga simu kumjulia hali, wala hajamuona tangu azaliwe, ana umri wa miaka miwili na nusu. hajamtia jicho wala kumuuliza.
Jee mama ana haki kubadilisha jina la mtoto huyu? asimpe jina la babake? Shukran kwa jawabu,
JazakAllaah, Wassalaam Aleikum
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa ndugu yetu muulizaji swali. Hakika swali
Ikiwa baba amemkana mtoto wake basi mtoto huyo hafai kuitwa kwa jina lake. Kwa ajili hiyo ndio baba akaona hana wajibu wakumtazama mtoto huyo kwa chochote. Baba anawajibika tu kumtazama mtoto wake ambaye ni damu yake.
Katika suala
Hivyo katika kubadilisha anaweza kumuita kwa jina lake au wanazuoni wamuite kwa jina la ‘Abdullaah kama jina la babake.
Na Allaah Anajua zaidi