Blood Donation: Muislamu Anaweza Kusaidiwa Kutiwa Damu Na Asiye Muislamu?

SWALI:

 

Assalaamu alakum warahmatullaahi wabarakaatuh,

 

Ni ipi hukumu ya Muislamu kusaidiwa damu na (kutiwa damu ya) mtu asiye-muislamu ambaye anatumia nyama na nguruwe au hatumii nyama ya nguruwe na vyakula vyengine haramu?

 

Je pana ulazima wa kutenganishwa damu inayohifadhiwa katika benki za damu (kuwekwa mbali kwa ile itakayotiwa Waislamu na ile itakayotumika kwa wasio-waislamu) wakati wa dharura na kuhami uhai?

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘Alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu ruhusa ya Muislamu kupata msaada wa damu kutoka kwa asiyekuwa Muislamu. Hakika ni kuwa hakuna katazo lolote kuhusu kutiwa damu kwa ajili ya matibabu. Inaruhusiwa kutiwa damu ya asiyekuwa Muislamu na ya Muislamu kusaidiwa asiyekuwa Muislamu kwa sababu ya kusaidia maisha ya mwanadamu. Masiha na uhai wa mwanadamu ni muhimu sana.

 

Msimamo wa Uislamu ni kuwa unafundisha Muislamu awe ni mwenye kumlisha mwenye njaa, kuwatizama wagonjwa na kuokoa maisha ya watu, yeyote awaye. Katika mas-ala haya hayatofautishi baina maisha ya Muislamu na asiyekuwa Muislamu.


Kitu cha muhimu cha kutizama ni je, damu inayotaka kutumiwa ni safi bila ya kuwa na viini kama vya ukiwmi au vinginvyo ambavyo vinaweza kudhuru afya na siha ya mwenye kupatia au vipi? Ikiwa damu hiyo ni hivyo basi yaweza kutumiwa bila ya shida.

 

Na Allaah Anajua zaidi.

 

 

Share