Sehemu Gani Ambazo Haipasi Kutoa Assalamu Alaykum?

SWALI:

 

Asalam allakum,

 

Ama baada ya kumshukuru Allah na mtume wake (salallah alaih wasalam) na masahaba wake na wafuasi wote, napenda kuuliza swali hili:

 

Nakumbuka nilipokuwa mdogo zamani moja kati ya darasa za msikitini niliwahi kumsikia sheikh wetu akisema kuwa kuna baadhi ya sehemu sio vizuri au haipaswi kutoa asalam allaykum, mfano kuamkia hivyo kwa mtu anayekula au anayesoma qur'an.  Jee hii ni kweli? Kama ni kweli sehemu nyengine zisizofaa kutoa asalam allaykum ni zipi.

 

Nakushuruni sana kwa msaada wenu. Inshaallah mola atakulipeni mema.

 


 

 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu sehemu zisizofaa kutoa salamu.

Ama kwa hakika ni kuwa sehemu ambazo Muislamu hafai kumtolea mwenziwe Salaam ni kama zifuatazo:

 

1.     Chooni.

2.     Kwa anayesoma Qur-aan.

3.     Kwa anayeswali.

4.     Kukatazwa kuwatolea salaam wanawake wasio Mahram zao,  na wao kuwatolea wanaume kuchelea fitna.

5.     Kuanza kuwatolea makafiri.

 

Hakuna katazo lolote la mtu kumtolea salaam mwenziwe anayekula.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

 

 

Share