Upigaji Kura Nini Hukmu Yake?

SWALI:

 

Assalam aleykum.. nimejitokeza tena katika ukumbi huu wa maswali lengo ni kutaka kutoka wasiwasi wangu wa moyo.. swali langu ni je. tunawajibika kupiga kura kama zifanyavyo nchi nyengine.. shukran sheikh wangu nina shauku ya kupata jibu la swali hili.. wabillahi tawfiki..

 


 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

 

Kwanza kabla hatujajibu swali lako, tunakukumbusha kuwa unapoandika jina la Allaah au Mtume, usifupishe mbele yake kwa kuweka (S.W.) au (S.A.W.) kama ilivyozoelekea na wengi, bali andika kwa kirefu maneno hayo bila ya kuyafupisha. Andika (Subhaanahu wa Ta’ala) baada ya kumtaja Allaah, na andika Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) au (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) baada ya kumtaja Mtume. Hivyo ndivyo inavyopaswa, na ndio heshima zaidi na utukufu na ndivyo inavyotamkwa na si kama inavyofupishwa na wengi kimazoea. 

 


 

Kuhusu swali lako ni kuwa wanazuoni wa sasa wamegawanyika makundi mawili kuna wanaopinga upigaji kura na wengine wenye kuunga. Kila mmoja anatoa dalili zake, na zinazoonyesha kuwa inafaa zina nguvu kwa kiasi chake. Majma’ al-Fiqhiy al-Islaamiy katika mwaka wa 2002 (1423 Hijri) walikutana kujadili suala hilo na wanazuoni 18 wanaotambulikana kutoka pembe takriban zote za dunia walipitisha kuwa inafaa baada kulijadili kwa mapana na marefu.

 

Na Allaah Anajua zaidi

Share