Ukimbizi - Watoto Wanashangazwa Baba Kubadilisha Jina Nifanyeje?
SWALI:
Natumae swala kama hili limeshaulizwa, lakini ningeomba ufafanuzi zaidi Inshallah. Mimi nimekuja ulaya kwa ukimbizi kwa kusema urongo kama tunavyosema kwa sababu ya maisha mazuri, ikanibidi ni badilishe jina langu lote baada ya kupawa fikra hiyo. Leo niko na mke na watoto na jina ninalo tumea siyo langu kwa kizazi, athari ninayo iyona ni kwa watoto kuitwa jina la baba ambalo wanajuwa kuwa siolake na wao wanajuwa jina asili langu,wanakuwa na utata ndani yake jee nifanye nini kutatua hali hino kwa njia ya Kiislam?
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa ndugu yetu muulizaji swali. Hali kama hiyo inajitokeza pindi mtu akikiuka agizo la Allaah Aliyetukuka na baada ya hapo inakuwa ni majuto na kutoweza kujirudi. Kwa hali hiyo ndiyo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akapiga vita
Kwa jinsi hiyo ndio kusema ukweli ukawa na ujira mkubwa
Maafa ya kusema uongo ni kama hayo yaliyokupata na kwa kupatwa na hilo hata watoto inakuwa ni vigumu kukuelewa na huenda hilo likawaathiri nao wakaingia katika kosa hilo la uongo. Ikiwa inawezekana kurekebisha kosa
Baada ya kufanya hivyo, itabidi urudi kwa Allaah Aliyetukuka kwa kuomba toba ya kikweli na uhakika, ujute kwa ulilolifanya na uweke azma ya kutorudia tena kosa
“Hakika mema huondoa maovu. Huu ni ukumbusho kwa wanaokumbuka” (11: 114).
Naye Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) anatuambia:
“Mche Allaah popote pale ulipo. Na ufuatilize jambo baya kwa zuri, litafuta
Tunakutakia kila la kheri na fanaka katika yote yatakayokupeleka katika mema na kupata msamaha kutoka kwa Allaah Aliyetukuka pamoja na kurekebisha hayo makosa.
Na Allaah Anajua zaidi