Kubadilisha Jina La Baba Inajuzu?
SWALI
asalam alaikum warahmatu llahi, baada ya salam na kumshukuru aza wajalah kwa rehma zake na mtume wetu mohammad (s.a.w) ninapenda kushukua nafasi hii kuuliza suala kuhusu jina la baba yako, kwani limekua linanitatiza tokea nilipoambiwa na wenzangu kua inasemekana kidini huruhusiwi kubadilisha jina la baba. Mimi ninaishi
JIBU:
BismiLLaah wa AlhamduliLLaah was-Swalaatu wa Salaamu ‘alaa Muhammad wa ‘alaa aalihi wa
Uislamu umekataza kubadilisha jina la baba na kutumia jina lolote jengine
((ادْعُوهُمْ لِآبَائِهِمْ هُوَ أَقْسَطُ عِندَ اللَّهِ))
((Waiteni kwa baba zao, maana huo ndio uadilifu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu)) [Al-Ahzaab: 5]
Aayah hii ileteremshwa baada ya Mtume صلى الله عليه وآله وسلم alipomchukua Zayd bin Haarith na kumfanya ni mtoto wa kupanga (adoption) ambaye baada ya hapo aliitwa Zayd bin Muhammad. Allaah سبحانه وتعالى Akataka kuondosha mila hiyo ya kumbadilisha mtu jina la baba yake, kwa hiyo baada ya kuteremka Aayah hii, akarudia kuitwa kwa jina lake la asili Zayd bin Haarith.
Na ndio maana hata kama Kafiri akibadilisha Dini, anaweza kubadilisha jina
Na tabia ya mke kubadilisha jina kutumia jina la mume, mfano kuitwa Mrs Juma, ni tabia zisizolingana na maadili na mafundisho ya Kiislam kabisa! Na
Kufanya hivyo vile vile kuna madhara yake.
Pili, inapotokea kifo cha mume au talaka, inabidi mke arudie kubadilisha pasipoti na vyeti vyake vyote vingine kuweka jina la baba badala ya jina mume, hivyo ni usumbufu unaompotezea mtu fedha na wakati wake.
Kwa hiyo Muislamu ni bora kubakia katika amri na mafunzo ya dini yake ili kupata ridha ya Mola wake na pia kujiepusha na usumbufu mbali mbali.
Na Allaah Anajua zaidi