Muislamu Kuingia Kanisani Inafaa?
SWALI:
Shukurani zote zina mustahiki Allah subhanahu wataalla!
Swali langu nikuhusu muislam kuingiya kanisani, nasi
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu kwa swali lako kuhusu kuingia katika Kanisa.
Hakika Uislamu haujamkataza Muislamu kuingia katika Kanisa ikiwa kuna udhuru wa kufanya hivyo. Ikiwa ni kujua wanayofanya Wakristo ili uwe na maalumati ya moja kwa moja kuhusiana na ‘Ibaadah zao au kwa shughuli nyingine kama msaada wa Waislamu kuwasaidia masikini waliokumbwa na misukosuko na wakapata hifadhi katika Kanisa.
Hata hivyo, si vyema kwa Muislamu kuingia katika chuo chochote kile
Tunaamini kuna vyuo vingi Ulaya ambavyo havina mambo ambayo umeyataja hayo kwa sharti la kuwa nesi. Hatujui vyuo vyote vinginevyo umeviacha na kuingia hicho chenye masharti
Hivyo tunakushauri ndugu yetu, uepukane na mambo ya haraam na mashaka mashaka katika Dini yako na utafute yale yenye usalama na Dini yako na kupata radhi za Allaah ambalo ndilo lengo kuu la kuwepo kwako hapa ulimwenguni.
Na Allaah Anajua zaidi