Mume Anashindwa Kurudisha Amana Ya Mke Aliyeachana Naye – Aombe Du’aa Gani Kuhusu Dhulma Aliyomfanyia?
SWALI LA
Bismilahi Arahmani Arahim. Asalaam alaikum warahmatullahi wabarakatu,
Kuna mtu na mkewe, yule mke kampa mumewe hela ili amuekee (amuhifadhie) yaani ni kila mwezi huyo mume anapewa amana hiyo amuekee huyo mkewe kwa muda wa miaka, mpaka zikatimia maelfu kadhaa. Kisha mke na mume wakaachana baada ya miaka 6. Mke kadai haki zake zile alizo mpatia mumewe ili umuekee hakulipwa, na akatumana kwa watu ili wamtetee adai haki zake alizo muamini kumpa mtalaka wake amuekee. Lakini Mume mwenyewe hajakataa
SWALI LA PILI:
Bismilahi arahmani arahim.
Asalaam alaikum warahmatulahi wabarakatu. Jee ikiwa mwanamke amempa mtalaka wake pesa amuekee kila mwezi kabla hawajaachana kwa muda wa miaka sita. Kisha walipo achana mume anamsumbua kumlipa mtalaka wake haki zake. Jee hukumu ya huyo Mume ni nini?
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho
.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu kumdai mtalaka wako pesa ambazo anasumbua kuzilipa.
Hii ni mojawapo ya dhulma ambayo wanawake wanafanyiwa katika jamii yetu. Inaonekana kama waume wameshindwa kuwa waaminifu kwa wake zao kwa wanachoamiwa kwa kiasi ambacho hata baada ya talaka wanapata usumbufu kutoka kwa watalaka wao.
Hii ni katika zile alama za unafiki kwa upande wa mwanamme, kwani alama ya mnafiki ni yule ambaye anapoaminiwa hufanya khiyana. Kisha hii dhulma itakuwa ni
Na hiyo mara nyingi hutokea kwa wanawake kwa kutojali kufuata maagizo ya Uislamu pindi wanapopata posa. Wazazi na wasichana wao huona kuwa hiyo ni kheri na hivyo kukubali mara moja bila ya kumchunguza.
Ama kuhusu du’aa hakuna du’aa maalumu lakini unaweza kuomba yoyote kwa lugha yoyote lakini hatari yake ni kuwa du’aa hiyo hairudishwi na Allaah Aliyetukuka. Hiyo ni ile iliyozungumziwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) ya kuwa du’aa ya mwenye kudhulumiwa haina pazia kwa Allaah Aliyetukuka. Kumuombea du’aa ni
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ قَالَ قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((ثَلَاثَةٌ لَا تُرَدُّ دَعْوَتُهُمْ, الْإِمَامُ الْعَادِلُ وَالصَّائِمُ حَتَّى يُفْطِرَ وَدَعْوَةُ الْمَظْلُومِ يَرْفَعُهَا اللَّهُ دُونَ الْغَمَامِ يَوْمَ الْقِيَامَةِ وَتُفْتَحُ لَهَا أَبْوَابُ السَّمَاءِ وَيَقُولُ بِعِزَّتِي لَأَنْصُرَنَّكِ وَلَوْ بَعْدَ حِينٍ))
Kutoka kwa Abu Hurayrah (رضي الله عنه) amesema: Mtume (صلى الله عليه وسلم) amesema: (([Watu] Watatu hairudishwi Du'aa zao; Imaam muadilifu, mwenye Swawm mpaka afuturu, na Du'aa ya aliyedhulumiwa, Anainyanyua Allaah bila ya mawingu Siku ya Qiyaamah and inafunguliwa milango ya mbingu na Anasema: Kwa Utukufu Wangu, Nitakunusuru japo baada ya muda)) [Ibn Maajah, Ahmad]
Sisi tunaona kuwa utumie njia kwanza za kupitia kwa watu wake ili mume alipe deni
Ama mume wakati alipokuwa amekuoa alikufanyia dhulma ya kutokupa chakula ni madhambi juu yake kwa kufanya hivyo na atakwenda kulipwa mbele Siku ya Qiyaamah kwa hayo. Hata hivyo ilikuwa ukamshitaki kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake, lakini
Tunamuomba Allaah Aliyetukuka Amtie fahamu mume huyo na aweze kurudisha amana hiyo yako.
Na Allaah Anajua zaidi