Mapenzi Ya Kujionyesha
SWALI:
Assalaam alaykum
Swali: naomba munisaidie katika swali langu hili,nilipokuwa na mumewangu, kila nnapotaka kuwa karibu nae hunikwepa, kwa kujidai anaudhu. Lakini nilikuwa nikihisi akiona wasichana wetu wa kazi wanakuja yeye hutaka kunikaribia, kitu ambacho mie sikupenda kitendeke mbele ya mtu yeyote .aliwahi kuniambia kuwa wakija watu tuwaoneshe kuwa tunapendana, nikamwambia mimi siwezi kuonesha watu,
Wassalaam alaykum wa rahmatullah
JIBU:
AlhamduliLlaah - Himdi Na Sifa Zote Anastahiki Allaah (Subhaanahu wa Ta’aala) Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani dada yetu kwa swali lako zuri. Ni muhimu kuwa tuelewe kuwa maumbile ya mwanadamu ni kuona haya na kutoweza kufanya lolote ambalo linakwenda kinyume na ada za maumbile yake. Baina ya mume na mke, mwanamke ndiye mwenye hayaa zaidi katika suala la kufanya chochote mbele ya watu. Qur-aan inatueleza habari za yule binti wa yule mzee mkongwe mcha Mngu pindi alipokwenda kumchukua Nabii Muusa (‘Alayhis Salaam) alipotumwa na babake. Allaah Aliyetukuka Anasema: “Basi akamjia mmoja wao katika wale wawili, anakwenda na huku anaona haya” (28: 25).
Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) naye anatuambia: “Ikiwa huoni hayaa basi fanya unalotaka”. Amesema tena: “Hayaa ni sehemu ya Imani” (al-Bukhaariy). Na pia, “Hayaa haiji ila kwa kheri”.
Mapenzi baina ya mume na mke yanafanywa wakiwa peke
Ni wazi kuwa mwanzo Allaah Aliyetukuka na Mtume wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) wamekataza kabisa watu kufanya amali kwa kujionyesha (Riyaa). Kufanya Riyaa kunamfanya Muislamu awe atakuwa ni mwenye kupata adhabu Siku ya Qiyaamah, kwani huwa hafanyi kwa ajili ya Allaah Aliyetukuka.
Nasaha yetu kwako awali ya yote ni wewe kuweza kumuweka mumeo chini na kumueleza hayo kinaganaga bila kuficha kwa sababu hiyo si tabia ya Muislamu mwema wa kuanza kumshika mke wake wakiwa wapo watu mbele na ikiwa hapana mtu basi kumkimbia na kutotaka kabisa kuwa karibu naye. Hilo ulilofanya dada yetu ni sawa sawa kwani munkari (uovu) unafaa uondoshwe kwa mkono, ikiwa mtu hawezi kwa mkono, basi kwa mdomo na ukishindwa kabisa, basi ni kuchukia moyoni na huo ni udhaifu wa Imani.
Kufanya hivyo hujamkosea kabisa katika haki bali ni kumfundisha haki zake ambazo anafaa azifahamu na asiwe ni mwenye kuvuka mipaka iliyowekwa na Sharia. Tunaona kwa tatizo
Tunakutakia kila la kheri na tawfiki katika kumrekebisha mumeo. Tunamuomba Allaah Amuondolee mumeo riyaa na mushikamane katika ya kheri na kuachana na yaliyo maovu.
Na Allaah Anajua zaidi