Wakwe Wanataka Kumuozesha Mke Mwengine Mtoto Wao Kisha Asiwe Ananipa Haki Kwa Sababu Ya Kuwa Mimi Sio Kabila Lao La Kihindi
SWALI:
Assalam Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh,
Ningependa mwanzo kuwashukuru sana kwa kazi yenu nzuri, Mashallah na kuwatakia nyote ndugu katika Islam mwaka mpya wa 1430 mwema wenye Barka na uwe mwaka wa kheri na uongofu kwetu sote, tumkurubie na kumtakasa Allah "Subhana Huwat' Allah" na tufuate yale yote aliyotufunza kipenzi chetu na Mtume wetu Muhammad, "Swalallahu Alaihi Wasallam".
Ndugu katika Islam, ningependa kuuliza swali ambalo ni ndefu na natarajia Insha'Allah mutanisaidia kwa jibu kwa haraka kadri ya Allah Subhana Huwat'Allah atakavyowaezesha.
Mimi nimeolewa na mume Muislamu wa kihindi na sasa tuna mtoto mmoja. Ndoa yetu hii imekuwa na mitihani mingi kwa sababu ingawa upande wa familia yangu hawana shida nayo, upande wa mume wangu haswa mamake mume wangu (mavyaa) amekuwa hana raha nayo kwa kile anachosema kuwa ndoa yetu haitodumu kwa sababu mwanawe (mume wangu) hakuoa mhindi mwenzao bali kanioa mimi. Tumekuwa na subra siku nyingi na kwa vile mume wangu anamheshimu mamake ambaye toka hapo waliishi pamoja, tuliamua mimi niishi kando naye aishi na mamake lakini huja kututembelea kila wiki kwani sote wawili twafanya kazi. Mimi naishi na mwanangu mchanga na msaidizi wangu ambaye humwangalia mtoto wetu wakati niko kazini. Nimestahamili haya kwa kuwa sitaki vita na mamake, lakini ni subra tu na kumpenda mume na mtoto wangu.
Hivi karibuni yule mama ambaye sasa ni mzee amekuwa na hasira nyingi kwa mume wangu kwa sababu hanitaki mimi na yeye na jamaa zako wanamwambia aoe mke mwingine wa kihindi na awachane nami lakini mimi na mume wangu hatuna matatizo yoyote, ni wao tu wenye mambo hayo mengi. Sasa hivi mume wangu yuko katika hali ya pressure nyingi kutoka kwa jamaa zake na ananiambia kuwa yeye hataki kuniwacha lakini tu kwa sababu ya kuwaridhisha watu wake haswa mamake anayehofia atamnyima radhi zake kwa kutomtii, ananiambia nimkubalie amuoe huyo mke atakaye lazimishwa kumuoa na jamaa zake. Sasa mimi nakubali kuwa Allah Subhana huwat'Allah amewaruhusu wanaume kuoa hadi wake wanne, lakini je ni haki katika hali
Nitashukuru
Shukran, Wajazakallahu Khair
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Ndugu yetu Allaah Akupe kila la kheri inaonyesha katika maneno yako karibu yote kuwa unaelewa mengi kuhusu dini yako ni jambo la kujivunia na Allaah Awape kila la kheri waliokufiksha hapo. Umesema, Mimi nimeolewa na mume Muislamu na hili ndio litakiwalo kwa kila mwanamke Muislamu ama kusema, wa kihindi, hili halina haja katika Uislamu wala kwa Muislamu.
Umeeleza kuwa, tuliamua mimi niishi kando naye aishi na mamake. Kama mlikubaliana na kuwa haki zako ulikubali zisipatikane kama mke na mume
Kisha ukasema, wanamwambia aoe mke mwingine wa kihindi, kuambiwa au kushauriwa aoe mke mwengine si jambo baya kama atalimudu na maelezo yako yanathibisha hayo na huu ndio Uislamu hata kama wewe utaona kuwa wewe ndio unapaswa umtafutie huyo mke basi
Ama kumshauri awachane nami, hili si katika mafundisho ya Uislam kwani kumchukiza mtu kwa mume wake au mume kwa mkewe ni jambo lenye kumtoa mtu katika kuwa miongoni mwa Waislamu wachilia mbali kumuachisha mtu kwa mumewe au kumtaka mume amuache mkewe haya ni katika yasiyokubalika katika Uislamu
Amesema Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Hayuko pamoja na sisi mwenye kumchukiza mwanamke kwa mume wake, au mtumwa kwa bwana wake.” Imepokelewa na Al-Haakim, kitabu cha twalaaq, amesema Hadiyth hii ni sahihi kwa sharti ya Imaam Al-Bukhaariy lakini Al-Bukhaariy hakuitoa kwenye Kitabu chake.
Ukasema, lakini tu kwa sababu ya kuwaridhisha watu wake haswa mamake anayehofia atamnyima radhi zake kwa kutomtii, Wazee hawana radhi za kumuachia wala chochote hayo ni maneno tu yaliyozooleka, mwenye radhi ni Allaah na kama yuko na heshima na anawahudumia wazee wake na kuwatii katika maarufu basi hakuna dhambi atakayoipata mtu kwa Mola wala hakuna wa kumuachia radhi; hivyo la muhimu ni yeye kumfanyia wema hasa huyo mama kama anavyotaka Allaah basi radhi zake Atapata mumeo kwa Allaah kwani Yeye ndiye mwenye kutoa na kuwachia radhi sio wazee wala mtu yeyote.
Ukaeleza, ananiambia nimkubalie amuoe huyo mke atakaye lazimishwa kumuoa na jamaa zake wewe kama unampenda huyo mumeo kama unavyodai basi huna haja ya kumkatalia lakini ni vyema wewe kama ni mkewe ambaye mmeshaishi pamoja na kuelewa matatizo ya maisha yenu leo mmepata na kesho hakuna kitu na hali yake inaielewa wewe na yeye mwenyewe basi mshauri na kumwekea wazi kila kitu kuhusu maisha yenu na namna ulivyokuwa ukimstahamilia kupata na kukosa; yawezekana mke huyo wa kihindi amepewa zawadi na hatakiwi kitu ila shughuli ya kitandani tu, sasa kukataa si jambo zuri ametunukiwa na anao uwezo wa kitanda lakini hana uwezo wa kinyumba kula kuvisha na kadhalika yote atasimamia mama au huyo mke au jamaa zake, na kama huyo mumeo ana akili zake na anaelewa ukweli kuhusu maisha na kuwa hana mbele wala nyuma basi ataweza kuwashauri jamaa zake kuhusu hali yake.
Ukaendelea kueleza, Sasa vipi leo alazimishwe kuoa, Hakuna mtu anayelazimishwa kuoa kwani kuoa siyo kupeleka mkono na kusema nimekubali kumuoa binti fulani, bali kuoa ni kumuingila huyo binti na
Umesema, lakini mimi nimemwambia akitaka kuoa mke kwa kulazimishwa, basi anipe talaka yangu, na hili hataki kusikia, Ndugu yetu hutakiwi kuomba talaka kwa sababu tu mumeo ameoa mke iwe kwa kulazimishwa au hata kwa kutunukiwa au kwa sababu yoyote ile isiyokubalika lakini wewe
Amesema Mjumbe wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): “Mwanamke yeyote atakayeomba talaka kwa mume wake bila ya sababu (inayokubalika) basi Allaah atamuharamishia kunusa harufu ya Pepo” Imepokelewa na Al-Haakim, kitabu cha twalaaq, amesema Hadiyth hii ni sahihi kwa sharti ya Shaykhayn -Imaam Al-Bukhaariy na Muslim- lakini wote wawili hawakuiweka kwenye vitabu vyao.
Na Allaah Anajua zaidi