Mke Wa Mwanzo Anamuekea Masharti Mumewe
SWALI:
Ahsante
kuna mtu ana wake wawili wote anawependa na anafanya kama sheria inavyotaka lakini mke mkubwa baada ya mke mdogo kujifungua alibadilika na kumwambia mumewe yafuatayo:
a) Uniache au umuache mwenzangu
b) usilale zamu
c) Ukimfata ndio talaka yangu
Jee sheikh mwanamke huyu aelezwe vipi ili ajue kama sheria ya uke wenza kaipanga Mungu kwani wanawake tupo wengi? Mke mdogo kamwambia mumewe mimi sipendi umuache mkeo hivyo wewe ishi
nyumba ndogo . Suali Sheikh, Mwanamke huyu asiejua sheria itakua vipi? Na ndoa hizi zitakuwa vipi? Na huyu mwanamke afanye vipi? Naomba majibu
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho
Shukran dada yetu kwa swali
Masharti katika Uislamu yanatakiwa yaende sambamba na anavyotaka Allah na Mtume Wake na kwenda kinyume na kauli zao ni kuingia katika ufasiki na udhalimu na hata katika ukafiri. Mtume (s.a.w.) amesema: “Hakuna kumtii kiumbe yeyote ikiwa katika
Mke au mume anakosa kujua sheria kwa kuwa ima malezi ya wazazi wao hayakuwa mazuri au hawakupata mafunzo ya msingi kabisa. Ndio Mtume Muhammad (s.a.w.) akahimiza
Ikiwa mke ni mchaMungu inakuwa ni rahisi kuweza kuelewa sheria ya Allah, lakini ikiwa ni kinyume na hivyo inakuwa ni matatizo makubwa
Kitu cha kufanya ni kujaribu kutumia mashoga zake au masheikh ili waende wakamnasihi na kumueleza
Katika kumpatia nasaha huenda akabadilika na akawa mke mzuri. Na katika kutoa hii nasiha inatakiwa zitumie njia na mbinu mbali mbali ili kumuelimisha na kumfahamisha na kutumike hekima na maneno matamu. Na nina yakini kuwa mke huyo wa mwanzo atakuwa ni mwenye kubadilika na ikawa ni faraja kwa wanandoa hao na familia zao.
Ikiwa mbinu zote zimetumika na hakuna natija yoyote basi itabidi talaka itoke na hapo mume ndiye atakayekuwa ni mwamuzi wa mwisho. Lakini tunaomba isifike hali hiyo.
Na Allah Anajua zaidi.