Mke Anafaa Kumtii Mume Asiyeswali?

SWALI:

 

 

If you remind someone like your husband to pray salat and he doesn’t pray until the time for that salah goes can I obey such a person.

 

 


 

 

 

 

JIBU:

 

Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho

 

 

Kuhusu mtu kutoswali, Hakika ni makosa makubwa kwa Muislamu kutoswali. Kukosa kuswali ni katika madhambi makubwa sana ambayo Muislamu anayafanya. Na kukosa kuswali kunampelekea mtu kuingia katika ukafiri na hivyo kustahiki kuingizwa Motoni. Ni jukumu lako kama mke kumnasihi mumeo kubadili maadili yake kwa kutekeleza Swalah. Ikiwa hatekelezi ni lazima uwe na kikao naye hasa ili umueleze umuhimu wa Swalah na madhambi ya kuiacha hiyo Swalah. Ikiwa atasikiliza itakuwa sawa na lau hatosikiliza itabidi upeleke kesi hiyo kwa wazazi wako, wazazi wake na nyinyi wawili muwepo kuzungumzia hilo na kufikia suluhisho kuhusu suala hilo kinaganaga.

 

Kutopatikana suluhisho lolote ni kuwa wewe kama mwanamke wa Kiislamu hufai kuishi na mume kama huyo. Inabidi uchague kuishi naye kinyume na maagizo ya Uislamu au kuachana naye. Kwa ajili hiyo itabidi uende kwa Qaadhi au Shaykh yeyote anayejulikana kwa uadilifu wake ili awapatie ufumbuzi wa kesi hiyo yenu.

 

Hata hivyo, tatizo kubwa linapatikana mpaka mwanamke wa Kiislamu akaolewa na Muislamu ambaye haswali ni kuwa hatukufuata maagizo ya Uislamu katika kuchaguana kabla ya ndoa.

 

Unaweza kumsaidia kwa kumchapishia makala katika kiungo kifuatacho apate kujua  zaidi umuhimu wa Swalaah.

 

Swalah, Umuhimu Wake, Fadhila Na Hukmu Ya Mwenye Kuacha 

 

Mume Hataki Kuswali Anasema Hana Muda Yuko Kazini

 

 

 

Tunakutakia kila la kheri katika mtihani na tunamuomba Allaah Amrudishe mumeo katika Uislamu kurudi kuliko kwema na kuzuri.

 

Na Allaah Anajua zaidi

 

Share