Nimeshindwa Kuvumilia Mume Wangu Kuoa Mke Wa Pili, Je Naweza Kudai Talaka?
SWALI:
Assalaam alaykum warahmatu llahi taala wabarakaatu. Swali langu ni hili: kama mumeo kaoa na alipokwambia ukakubali na ukastahamili lakini kila ukikaa unajiona huna uwezo wa kustahamili unaumia
JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola Mlezi wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu ‘anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Shukrani zetu za dhati kwa swali lako kuhusu uke wenza.
Awali ya yote tunakupongeza
Hata hivyo, yaonyesha baadaye umeshindwa kuendelea na
Kwa hali moja au nyingine ikiwa mume ameegemea upande mmoja kwa kumpendelea mke wa pili (au mdogo) inatakiwa utumie njia za kisheria kuweza kupata haki zako za uke. Ikiwa hupatiwa basi utumie njia za kisheria kuweza kuzidai na ikiwa mume amekaidi utakuwa na haki ya kudai talaka.
Na ikienda kuwa unaona huoni raha bila ya makosa yoyote kutoka kwa mumeo unaweza kuomba talaka kwa sharti umrudishie mumeo huyo mahari aliyokupatia. Na hiyo inaitwa Khul’u katika sheria.
Bonyeza viungo vifuatavyo upate maelezo zaidi kuhusu mas-ala haya:
Sababu Gani Zinamruhusu Mke Kuomba Talaka?
Hata hivyo, nasaha yetu kwako ni ubakie katika ndoa yako, kwani waume hawapatikani kwa rahisi hasa wale ambao ni wema.
Tunakutakia kila la kheri katika kubakia katika ndoa hiyo yako. Na Allaah Aliyetukuka Akupatia mafanikio mema.
Na Allaah Anajua zaidi